Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt.
Samia Suluhu Hassan akizungumza na Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Mambo ya Nje
wa Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE), Mhe. Abdullah Bin Zayed Al Nahyan tarehe 05
Mei, 2025 Ikulu jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt.
Samia Suluhu Hassan akiwa na Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Mambo ya Nje wa
Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE), Mhe. Abdullah Bin Zayed Al Nahyan,
wakishuhudia utiaji saini wa Hati ya Makubaliano baina ya Wizara ya Afya na
Wizara ya Mambo ya Nje ya Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE) kuhusu uwezeshaji wa
ujenzi wa Hospitali ya The Emirates – Tanzania Bukoba mkoani Kagera, tarehe 05
Mei, 2025 Ikulu jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt.
Samia Suluhu Hassan akiwa na Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Mambo ya Nje wa
Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE), Mhe. Abdullah Bin Zayed Al Nahyan,
wakishuhudia utiaji saini wa Hati ya Makubaliano baina ya Serikali ya Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE) kuhusu ushirikiano
katika uwekezaji kwenye sekta ya madini, tarehe 05 Mei, 2025 Ikulu jijini Dar
es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt.
Samia Suluhu Hassan akiwa pamoja na Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Mambo ya Nje
wa Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE), Mhe. Abdullah Bin Zayed Al Nahyan,
wakishuhudia utiaji saini wa Hati ya Makubaliano baina ya Shirikisho la Vyama
vya Biashara na Viwanda vya UAE na Barazala la Taifa la Biashara kuhusu
uanzishwaji wa Baraza la Pamoja la Biashara kati ya Umoja wa Falme za Kiarabu
na Tanzania tarehe 05 Mei, 2025 Ikulu jijini Dar es Salaam.
No comments:
Post a Comment