Habari za Punde

Ziara ya Katibu Mkuu wa CCM Mkoa wa Kaskazini B,Unguja

 
 Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi Ndg Abdulrahaman Omar Kinana akipokelewa na dufu wakati akiwasili katika Wilaya ya Kaskazini B, Unguja kuaza ziara yake katika wilaya hiyo baada ya kupata maelezo ya utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM.
 Katibu Mkuu wa CCM akisalimiana na Wananchi wa jimbo la Donge baada ya kuwasili katika Tawi la CCM Donge Kipange. 
Mbunge wa Jimbo la Donge akitowa maelezo ya utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi kwa Katibu Mkuu wa CCM Ndg. Abdulrahaman Kinana wakati alipowasili katika jimbo hilo kujionea utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM kwa Wananchi wa jimbo lake.  
Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi Ndg Abdulrahaman Omar Kinana akimkabidhi mabati Mwalimu Mkuu wa Skuli ya Maandalizi Donge Kipange Bi Salma Suleiman, mabati hayo yametolewa na Mbunge wa Jimbo hilo Mhe Sadifa Juma Khamis.
Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi Ndg. Abdulrahaman Omar Kinana, akizungumza na Viongozi wa Chama wa Halmashauri za Wilaya na Mkoa wakati wa kupokea taarifa ya utekelezaji wa Ilani ya Uchgaguzi ya Wilaya ya Kaskazini B Unguja. wakiwa katika um
Katibu Mkuu wa CCM Ndg Abdulrahaman Kinana akimsikiliza Mwenyekiti wa Kikundi cha Ushirika wa Wanawake kinachojishughuliza na Utengenezaji wa Sabuni na mafuta.
Katibu Mkuun wa CCM Ndg. Abdulrahman Kinana akiangalia moja ya bidhaa zinazozaliwa na kikundi hicho wakati alipowatembelea na kuwachangia shilingi milioni mbili kusaidia kikundi hicho. 
Holi la kufanyia mitihani katika Skuli ya Sekondari ya Mahonda linalojengwa kwa nguvu za Wananchi na Mbunge na Mwakilishi wa jimbo la Donge.
Mwalimu wa Skuli ya Sekondari ya Mahonda akisoma risala ya ujenzi wa Hall hilo linalojengwa kwa nguvu za wananchi. wakati wa ziara yake kutembelea miradi ya wananchi. 
Katibu Mkuu wa CCM Ndg. Abdulrahaman Kinana akiwahutubia Wanafunzi wa Skuli ya Sekondari ya Mahonda, wakati wa ziara yake kutembelea miradi ya wananchi na kuangalia utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi. 
Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi Ndg. Abdulrahaman Omar Kinana akimkabidhi saruji mifuko 50,Mwenyekiti wa Kamati ya Skuli ya Sekondari Mahonda Ndg Salum Gharib Salum, mwanachama wa (CUF), Iliyotolewa na Mbunge wa Jimbo la Donge Mhe. Sadifa Juma Khamis, 
Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi Ndg. Abdulrahaman Kinana, akishiriki katika ujenzi wa Taifa ya ujenzi wa Hall la mitihani la skuli ya sekondari mahonda akiwa na mbunge wa jimbo la Donge Mhe. Sadifa Juma Khamis.
Katibu Mkuu wa CCM Ndg. Abdulrahaman Kinana, akimkabidhi Kiongozi wa Kikundi cha Ushirika katika jimbo la Kitope jumla ya Vikundi 32 vimekabidhiwa fedha taslim shilingi 400,000/- kila kimoja.  
Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi Ndg. Abdulrahaman Kinana akimkabidhi seti ya Camera Mwalimu Chuo cha Uandishi wa Habari cha Jimbo la Kitope vifaa hivyo vimetolewa na Mbunge wa Jimbo hilo Mhe Balozi Seif Ali Iddi.
Katibu Mkuu wa CCM akimkabidhi jiko la gesi Mwalimu wa Chuo Mafunzo ya Upishi kilichoko katika jimbo la Kitope Unguja.  
Katibu Mkuu wa CCM Ndg. Abdulrahaman Kinana akionja moja ya mapishi wanayojifunza Vijana wa Jimbo la Kitope akiwa na Mbunge wa Jimbo hilo la Kitope Mhe Balozi Seif Ali Iddi.
Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi Ndg Abdulrahaman Kinana akizindua Blog ya Jimbo la Kitope, wakati wa ziara yake hiyo katika Wilaya ya Kaskazini B.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.