STATE HOUSE ZANZIBAR
OFFICE OF THE PRESS SECRETARY
PRESS RELEASE
Zanzibar
16.2.2015

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la
Mapinduzi Mhe. Dk. Ali Mohamed Shein amendelea kusisitiza haja kwa Wakuu wa Mikoa na Wilaya kutoa taarifa kwa
wananchi kupitia vyombo vya habari ili wajue mambo yanayofanywa katika Mikoa na
Wilaya zao.
Dk. Shein
aliyasema hayo leo huko Ikulu mjini Zanzibar katika mkutano kati yake na
Uongozi wa Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Idara Maalum za SMZ, ulio kuwa na
lengo la kuangalia Utekelezaji wa Malengo ya Wizara hiyo kwa robo mbili kati ya Julai hadi Disemba 2014.
Dk. Shein alisema
kuwa huo ni utaratibu uliowekwa na Serrikali hivyo viongozi hao wanatakiwa
kutoa taarifa kwa wakati uliopangwa ili wananchi wajue mambo yaliyofanywa na
Mikoa, Wilaya zao sambamba na kujua juhudi za maendeleo zinazochukuliwa na Serikali katika maeneo hayo.
Aidha, Dk. Shein
alitumia fursa hiyo, kuwaeleza Wakuu wa Mikoa, Wilaya na Makatibu Tawala pamoja
na viongozi wote husika kuwa tayari Sheria muhimu zimeanza kufanya kazi na kwa
upande wao wanakila sababu ya kuzisoma na kuzifahamu kwa lengo la kuwasaidia
katika utendaji wao wa kazi ikiwemo Sheria ya Kuongoza Tawala za Mikoa na
Sheria inayoongoza Serikali za Mitaa.
Dk. Shein alisema
kuwa Sheria hizo zote zina lengo moja na ziko chini ya Ofisi ya Rais Tawala za
Mikoa na Vikosi vya SMZ. Pia, Dk. Shein alisisitiza haja ya uongozi wa Mkoa na
Wilaya kutoa taarifa juu ya suala zima la ulinzi na usalama kwa Ofisi yao.
Pamoja na hayo,
Dk. Shein aliusisitiza uongozi wa Mikoa na Wilaya kuwa na malengo katika
kutekeleza Kampeni ya miaka miwili ya kupinga udhalilishaji wa wanawake na
watoto sambamba na kuweka utaratibu wa kusimamia katika ngazi za Mikoa, Wilaya
hadi Shehia kwani hali ikenda vizuri Kampeni hiyo itafanikiwa.
Dk. Shein pia,
aliutaka uongozi wa Mikoa na Wilaya kuoa taarifa juu ya hali ya chakula, lishe
na hali ya usalama wa chakula hatua ambayo alieleza kuwa itasaidia kujua suala
zima la chakula hapa nchini.
Sambamba na hayo,
Dk. Shein aliwataka Wakuu wa Mikoa na Wilaya pamoja na Makatibu Tawala kutotumia muda mwingi kukaa maofisini na
badala yake waende kwa wananchi hatua ambayo itasaidia kwa kiasi kikubwa kupata
habari mbali mbali na kuwasaidia katika utendaji wao wa kazi.
Aidha, Dk. Shein
alirejea kauli yake ya kutaka vijana kushajiishwa juu ya suala zima la ajira na
kuitaka Mikoa na Wilaya kuwa na mipango ya kuwasaidia vijana huku akiushauri
uongozi wa Mikoa na Wilaya kushirikiana na Wizara ya Uwezeshaji, Ustawi wa
Jamii, Vijana, Wanawake na Watoto katika kuwasaidia vijana juu ya suala la
ajira.
Alisema kuwa
uongozi huo kwa mashirikiano ya pamoja kuwaeleza na kuwapa ushauri vijana sambamba
na kuwasaidia kuwapa taaluma juu ya suala zima la ajira ambapo pia, tayari
Serikali kwa upande wake imeshachukukua juhudi za makusudi kuanzisha Mfuko wa
Uwezeshaji ambao umekuwa ukiwasaidia vijana, kuwapa elimu pamoja na mambo
mengineyo katika kutafuta ufumbuzi wa changamoto hiyo.
Dk. Shein
alitumia fursa hiyo kuungana na Makamu wa Pili wa Rais Balozi Seif Ali Idd,
Katibu Mkuu Kiongozi na Katibu wa Baraza la Wawakilishi Dk. Abdulhamid Yahya
Mzee kutoa pongezi kwa Ofisi hiyo kwa
mafanikio makubwa iliyoyapata ikiwa ni pamoja na mpango mzuri wa Utekelezaji wa
Mpango Kazi wa Ofisi hiyo.
Mapema akisoma
muhtasari wa Utekelezaji wa Majukumu kwa miezi sita ya mwanzo ya mwaka wa
fedha kuanzia Julai hadi Disemba
2014/2015, Waziri wa Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Idara Maalum za SMZ Mhe.
Haji Omar Kheir alieleza majukumu,
muundo na utekelezaji wa Ofisi hiyo kati ya Julai hadi Disemba 2014.
Aidha, Waziri
Kheir alitoa shukurani kwa Dk. Shein kutokana na miongozo na maelekezo anayotoa
kwa Ofisi hiyo mara kwa mara kwa lengo la kufanikisha utekelezaji wa majukumu
yao ambayo yameweza kusaidia kwa kiasi kikubwa katika utekelezaji wa kazi zao.
Aidha, Waziri
Kheir alitua fursa hiyo kutangaza rasmin kuwa Sheria tatu muhimu zimeshaanza
kufanya kazi rasmin tokea jana ikiwemo Sheria ya Wakala wa JKU, Sheria ya
Kuongoza Tawala za Mikoa na Sheria inayoongoza Serikali za Mitaa.
Katika Mkutano
huo Makamu wa Pili wa Rais Balozi Seif Idd alihudhuria.
Rajab Mkasaba, Ikulu
Zanzibar
Postal Address: 2422 Tel.:0777427449. Fax: 024
2231822
E-mail:
rajabmkasaba@yahoo.co.uk
No comments:
Post a Comment