Habari za Punde

Dkt. Bilal Amfariji Jaji Mstaafu Augostino Ramadhani kwa kufiwa na Mama yake Mzazi.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mohammed Gharib Bilal akizungumza na Jaji Mkuu mstaafu Agostino  leo alipomtembelea nyumbani kwake kimara kwa ajili ya kumfariji kutokana na kufiwa na mama yake mzazi.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mohammed Gharib Bilal akisaini kitabu cha kumbukukmbu kufuatia kifo cha mama mzazi wa Jaji Mkuu mstaafu Agostino Ramadhani nyumbani kwake Kimara, alipofika kwa ajili ya kumfariji.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mohammed Gharib Bilal akiwafariji wana familia ya Jaji Mkuu mstaafu Agostino Ramadhani alipomtembelea nyumbani kwake Kimara kutokana na kufiwa na mama yake mzazi.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiagana na Jaji Mkuu mstaafu Agostino Ramadhani Baada ya kumfariji kutokana na kufiwa na mama yake mzazi alipomtembelea nyumbani kwake Kimara(Picha na OMR)


No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.