Habari za Punde

Ujumbe wa Manispaa ya Kiruna Wawasili Zenj leo

Ujumbe wa Manispaa ya Kiruna umewasili leo na kupokelewa na Afisa Tawala mstaafu wa Wilaya ya Kusini ambaye pia ni Makamo Mwenyekiti wa Kamati ya Wadi za Makunduchi, ndugu Abdallah Ali Kombo. Ujumbe huo utaanza ziara yake rasmi kesho kwa kuangalia kiwanja kinachotegemewa kujengwa chuo cha biashara huko kigaeni Makunduchi. Katika picha kutoka kulia ni ndugu David, Bi Anniken, ndugu Kenneth, ndugu Abdallah Ali Kombo na ndugu Ove, ambaye ndiye mkuu wa miradi.
Ujumbe kutoka Mji wa Manispaa ya Kiruna wawasili. Kwenye uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume ukiongozwa na Bi Jenny na Bwana Ove wakijitayarisha kuondoka uwanjani na kuelekea Makunduchi ambako wenyeji wao ni Kamati ya Wadi za Makunduchi

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.