Ujumbe mzito wa watu 6 kutoka Manispaa ya Kiruna nchini Sweden unatarajiwa kuwasili nchini Jumatatu, tarehe 16 mwezi huu kwa ziara ya wiki moja. Ujumbe unawasili nchini kufuatia ziara za kikazi za kutembeleana kati ya Wadi za Makunduchi na Manispaa hiyo. Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na mkuu wa miradi ya mashirikiano ya pande hizo mbili, ndugu Mohamed Muombwa ujumbe huo utafanya mazungumzo na wenziwao wa Makunduchi kuhusu kuongeza muda wa mradi wa kuwasomesha wanawake wa Makunduchi ujasiriamali pamoja na kuimarisha kituo cha kompyuta cha Makunduchi ili kiweze kutoa mafunzo kwa vijana wengi zaidi. Kwenye picha ndugu Mohamed Muombwa anazungumza na mkuu wa walimu kutoka Kiruna hapo afisini kwake Tunguu kuhusu ratiba ya ugeni huo
SERIKALI YAENDELEA KUIMARISHA UONGOZI NA USIMAMIZI WA ELIMU KUPITIA MAFUNZO
KWA VIONGOZI WA SHULE
-
NA EMMANUEL MBATILO, MICUZI TV
SERIKALI kupitia Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia imeendelea
kuimarisha uongozi na usimamizi wa elimu nchini kwa kutoa...
6 hours ago
No comments:
Post a Comment