
Pichani kulia ni Mhe. Omar Mjenga, Balozi Mdogo wa Tanzania Dubai, akimkaribisha Mhe. Aboud, Dubai, na kushoto ni Nd. Islam Balhabou
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Mhe. Mohammed Aboud, amewasili Dubai kwa ziara ya kikazi.
Akiwa Dubai, Mhe. Aboud atafanya mazungumzo na Kamati ya Maandalizi ya Maonyesho ya Biashara ya Dunia 2020 (World Expo2020).
Aidha, atafanya mazungumzo na Nd. Islam Balhabou, Mfanyabiashara Mtanzania ambaye amejitolea kufungua afisi ya biashara ya Zanzibar (Trade Mission).
Kwani lazima mvae kanzu mkienda Arabuni.Wewe ungelivaa msuri tu kwani ndio asili ya kigunya
ReplyDeleteWatu wanasema ukiwa ugenini,jaribu kuishi kama wenyeji wa hiyo nchi,kwa hiyo Bw. Aboud hajaharibu kitu,na juu ya hayo kwa wazanzibari kanzu ni kivazi cha kawaida.Muhimu ni kutafuta maslahi mazuri kwa wazanzibari.
ReplyDelete