Habari za Punde

Ujumbe wa Manispaa ya Kiruna kutoka Sweden watembelea eneo linapendekezwa kujengwa chuo cha biashara

 Ujumbe wa Manispaa ya Kiruna wakiangalia eneo la kujenga Chuo kwa umakini
Ujumbe wa Manispaa ya Kiruna, Sweden waanza ziara ya kikazi Makunduchi ambapo wametembelea eneo linalopendekezwa kujengwa Chuo cha biashara, kitengo cha chuo kikuu huria cha Tanzania, maktaba ya kisasa na vitengo vyengine vya kutoa elimu. Kwenye picha muwekezaji mzalendo wa Makunduchi ndugu Ali Jussa akimuonyesha eneo la kujengwa chuo hicho ndugu Ove mwenye miwani nyeusi. Ndugu Ove ni mkuu wa miradi ya mashirikiano kati ya wadi za Makunduchi na Manispaa ya Kiruna. Wengine katika picha ni wajumbe wa Kamati ya wadi za Makunduchi

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.