Habari za Punde

Dk Shein avishukuru vikosi vya ulinzi na usalama

STATE HOUSE ZANZIBAR
OFFICE OF THE PRESS SECRETARY
PRESS RELEASE
    Zanzibar                                                   28 Machi, 2015
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein amevishukuru Vikosi vya Ulinzi na Usalama vilivyoshiriki Gwaride la Kutimiza Miaka 51 ya Mapinduzi ya Zanzibar tarehe 12 Januari, 2015.

Akizungumza kwa niaba ya Mheshimiwa Rais, Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Ikulu na Utawaka Bora Dk. Mwinyihajihaji Makame Mwadini, alisema vikosi hivyo vilishiriki kikamilifu na kuweza kufanikisha sherehe hizo ipasavyo.

Katika hafla fupi ya chakula cha mchana iliyofanyika katika Kambi ya Jeshi la Wananchi Bavuai Migombani, mjini Unguja kwa ajili ya vikosi hivyo, Dk. Mwinyihaji alibainisha kuwa wakati wote kuanzia maandalizi hadi siku ya sherehe vikosi hivyo vilionesha ushirikiano mkubwa hadi kufanikisha sherehe.

Hafla hiyo ilihudhuriwa pia na Makamu wa Kwanza wa Rais Maalim Seif Sharif Hamad na Makamu wa Pili wa Rais Balozi Seif Ali Idi.

Sherehe za Maadhimisho ya Miaka 51 ya Mapinduzi zilifikia kilele chake tarehe 12 Januari, 2015 katika uwanja wa Amaan na kujumuisha shughuli mbalimbali likiwemo gwaride rasmi kutoka vikosi vya Ulinzi na Usalama.


Postal Address: 2422 Tel.+255 776 613 015, Fax: 024 2231822 

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.