MWANDISHI wa Habari wa Shirika la Magazeti ya
Serikali Zanzibar Ofisi ya Pemba, Haji Nassor Mohamed akitoa maelezo kwa
waandishi wa habari kutoka vyombo mbali mbali vya habari, katika kikao cha
kutathmini juu ya utendaji wa kazi za waandishi hao, mkutano huo uliofanyika
katika ukumbi wa Habari Maelezo Pemba.(Picha
na Abdi Suleiman, PEMBA.)
WAANDISHI wa Habari kutoka vyombo mbali mbali vya
habari kisiwani Pemba, wakisikiliza maelezo kutoka kwa mwandishi wa habari
mwandamizi kisiwani Pemba, Haji Nassor Mohamed katika kikao cha kutathmini
utendaji wa kazi za waandishi huko katika ukumbi wa Habari Maelezo Pemba.(Picha na Abdi Suleiman, PEMBA.)
MRATIB wa Tume ya Utangazaji Pemba, Afani Othman
Juma akitoa nasaha zake kwa waandishi wa habari kutoka vyombo mbali mbali vya
habari, huko katika ukumbi wa Habari Malezo kisiwani Pemba.(Picha na Abdi Suleiman, PEMBA.)
MWENYEKITI wa kikao cha waandishi wa habari kutoka
vyombo mbali mbali vya habari Pemba, ambae pia ni mwenyekiti wa Pemba Press
Club (PPC) Khatib Juma Mjaja akitoa nasaha zake kwa waandishi wa habari huko
katika ukumbi wa Habari Maelezo Pemba.(Picha
na Abdi Suleiman, PEMBA.)
MKUU wa shirika la magazeti ya Serikali ya Zanzibar
Ofisi ya Pemba, Bakar Mussa Juma akizungumza katika mkutano na waandishi wa
habari kutoka vyombo mbali mbali vya habari kisiwani Pemba, huko katika ukumbi
wa Habari Maelezo Pemba.(Picha na Abdi
Suleiman, PEMBA.)
No comments:
Post a Comment