Habari za Punde

Kumalizika kwa mafunzo ya siku tatu juu ya kukabiliana na ugonjwa wa Ebola

Mkuu wa kitengo cha kufuatilia mwenendo wa maradhi Zanzibar Dkt. Salma Masauni akitoa neno la shukrani mara baada ya kumaliza mafunzo ya siku tatu juu ya kukabiliana na ugonjwa wa Ebola, mafunzo hayo yamezaminiwa na Shirika la Afya la Umoja wa Mataifa (WHO) huko Hoteli ya Zanzibar Beach Resort.


Mwakilishi kutoka shirika la Afya la Umoja wa Mataifa (WHO)Tanzania Dkt. Grase Saguti akiwataka wafanyakazi wa sekta ya Afya Zanzibar kuyatumia vyema mafunzo waliyoyapata.



Naibu Waziri wa Afya Zanzibar Mhe. Mahmoud Thabit Kombo akiyafunga mafunzo ya siku tutu ya kukabiliana na ugonjwa wa Ebola, mafunzo hayo yanafanyika Hoteli ya Zanzibar Beach Resort Mjini Unguja. Picha na Makame Mshenga- Maelezo Zanzibar.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.