Na
Miza Kona na Maryam Kidiko-Maelezo Zanzibar 17/03/2015
Serikali
ya Mapinduzi ya Zanzibar imesema ina lengo la kuinua vipaji vya wasanii wa
Zanzibar ili kuhakikisha kuwa kazi zinazotokana na jasho lao zinakuwa sehemu ya
ajira kwao ili kuondosha usumbufu wanaoupata.
Hayo
ameyasema Naibu wa Waziri wa Habari wa Utamaduni Utalii na Michezo Bihindi
Hamadi Khamis wakati akijibu suala la Mhe. Wanu Hafidh
Ameir Nafasi za Wanawake aliyetaka kujua
kwa namna gani studio ile imewasaidia wasanii wa Zenj fleva kuinua vipaji vyao
kama vile studio ya Tanzania Bara.
Amesema
Wizara ya Habari, Utamaduni Utalii na Michezo ilijenga studio ya Rahaleo kwa ajili ya
Wasanii waliopo Zanzibar wakiwemo Wasanii wa Maigizo, Zenj fleva na wasanii wa
Taarab kwa kuinua vipaji vyao ili kuona kwamba
wanafaidika na kuweza kupata ajira.
“Vifaa vya kurikodia vimefika wiki iliyopita
bado vipo uwanja wa ndege kwa hatua ya kuvitoa na mafundi kutoka nje ya nchi
watakuja mwisho wa mwezi huu kwa hatua ya kuvifunga na tunatarajia wakimaliza
tu studio itaakuwa tayari kufanya kazi ya kurikodi na wasanii wetu watafaidika
na kazi zao”, amefahamisha Naibu huyo.
Amefahamisha
kuwa serikali inaendelea kuwasaidia wasanii wote waliojisajili katika Baraza la
Sanaa kwa kuwapatia mafunzo ya kuendeleza sanaa zao kupitia warsha na semina
kwa lengo la kuwapatia ujuzi wa kazi zao katika tasnia yao hiyo.
Ameeleza
kuwa serikali kupitia Wizara yake ya Habari Utamaduni na Utalii na Michezo
inaendelea kuwaelimisha wasanii wake kusajili kazi zao katika Jumuiya ya Haki
miliki (COSOZA) kwa ajili ya kudhaminiwa haki zao za uzeeni.
PIa Wizara inawapatia wasanii hao taaluma za
kufanya kazi zao katika kuandika, kurikodi na kufanya mauzo kwa lengo la
kufaidika na sanaa yao hiyo.
Wakati
huo huo Baraza la Wawakilishi limepitisha Mswada wa Sheria ya Miradi ya
Maridhiano Namba 1ya 1999 na Kutunga Sheria Mpya kwa ajili ya Kuanzishwa na
Kuendesha Mashirikiano baina ya Sekta ya Umma na Binafsi na Mambo Mengine
yanayohusiana na Hayo.
IMETOLEWA
NA HABARI MAELEZO-ZANZIBAR
No comments:
Post a Comment