Habari za Punde

Balozi Seif Afungua Mafunzo ya Miezi Mitatu ya Teknolojia ya Habari na Mwasiliano Zenj.

 Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akisalimiana na Mkuu wa Mafunzo ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano Zanzibar Nd. Abdullah Othman Ali wakati wa hafla ya kuyafunga mafunzo hayo hapo Skuli ya Sekondari Donge Mkoa wa Kaskazini Unguja. Kati kati yao ni Mbunge wa Jimbo la Donge Mheshimiwa Sadifa Juma Khamis, na nyuma ya Balozi Seif ni Mratibu wa Mradi unaoondesha mafunzo hayo Nd.Abdi Hamid Abeid.
 Mkuu wa Mafunzo ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano Zanzibar Nd. Abdullah Othman Ali akimpatia maelezo Balozi Seif wakati alipotembelea Darasa la mafunzo hayo hapo Skuli ya Sekondari Donge.
 Baadhi ya Wanafuzi wa Darasa la Teknolojia ya Habari na Mawasiliano Zanzibar wakishuhudiwa na Balozi Seif wakiendelea kufanya mazoezi ya vitendo katika kukabiliana na matatizo madogo madogo yanayojichomoza wakati wa matumizi wa kompyuta zao.
 Mmoja wa Wanafunzi wa Darasa la Teknolojia ya Habari na Mawasiliano Zanzibar akiperuzi kuangalia nini kimejiri duniani kupitia mtandao wa Internet akishuhudiwa na Balozi Seif.
 Baadhi ya Wananchi na Wanafunzi wakisikiliza Hotuba ya Mgeni rasmi Balozi Seif hayupo pichani wakati akiyafunga mafunzo ya miezi mitatu ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano Zanzibar hapo Skuli ya Sekondari Donge.
Balozi Seif akimkabidhi Cheti Mwenyekiti wa Jumuiya Kupambana na changamoto na kuwaendeleza Vijana Zanzibar Bibi Umukulthum kwa kusaidia uendeshaji wa mafunzo ya Teknolijia ya Habari na Mawasiliano. Kati kati yao ni Mwenyekiti wa Umoja wa Madereva na Utingo Zanzibar Maalim Khamis Mussa, na kushoto ya Balozi Seif ni Mratibu wa Mradi wa Mafunzo ya Teknolijia ya Habari na Mawasiliano Abdi Hamid Abeid na Mkuu wa Mafunzo hayo Nd. Abdulla Othman Ali.
Balozi Seif akiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa Jimbo la Donge, walimu na wanafunzi wa mafunzo ya Teknolijia ya Habari na Mawasiliano yaliyokuwa yakifanyika katika skuli ya Sekondari ya Donge. Kushoto ya Balozi Seif ni Mwakilishi wa Jimbo la Donge ambae pia ni Waziri wa Elimu Mh. Ali Juma Shamuhuna, Mratibu wa Mradi wa Mafunzo ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano Abdi Hamid Abeid na Mwenyekiti wa Jumuiya ya ZAFAYCO Bibi Umukulthum. Kulia ya Balozi Seif ni Mbunge wa Jimbo la Donge Mh. Sadifa Juma Khamis, Mkuu wa Mafunzo ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano Zanzibar Nd. Abdullah Othman Ali pamoja na Mwenyekiti wa Umoja wa Madereva na Utingo Zanzibar Maalim Khamis Mussa.( Picha na Hassan Issa – OMPR)

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.