Habari za Punde

Matukio ya Picha Mitaani Zenj.

Wanafunzi wa Skuli ya Sekondari ya Michakaeni Pemba wakiwa katika harakati za kupanda Meli ya Sea Link, baada ya kumaliza ziara ya kimasomo yaliofanya katika Kisiwa cha Unguja wakiwa wageni wa Skuli ya Sekondari ya Bububu , ziara kama hizi zinajenga uelewa kwa Wanafunzi kuelewa historia ya Visiwa vya Unguja na Pemba wakiwa katika ziara kama hizi za kimasomo katika pande mbili hizi za Zanzibar
Wananchi wa eneo la betras wakiangali  gari ya abiria yenye namba za usaji Z149 ER, ilioyopata ajali baada ya kugongana na gari ya Noah, iliotokea usiku kwa mujibu wa mashuhuda wa ajali hiyo, wamesema ajali hiyo imetokea majira ya saa 6 usiku.

Katika ajali hiyo watu waliokuwemo katika gari hiyo wameumia na kukimbizwa hospitali kuu ya mnazi mmoja kwa matibabu

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.