Habari za Punde

Pamoja na kuakhirishwa kwa kura ya maoni, Katiba inayopendekezwa kusambazwa kwa njia ya sauti nchi nzima





Pamoja na Tume ya  Taifa ya Uchaguzi kuahirisha  tarehe ya kupiga kura ya maoni, Shirika la Kimataifa linaloshughulikia Elimu na Utamaduni (UNESCO), kwa kushirikiana na Kampuni ya Focus Media pamoja na Mtandao wa radio za jamii  (COMNETA), limeamua kusambaza Katiba inayopendekezwa kwa njia ya sauti nchi nzima, ili wananchi wapate elimu  kuhusu maudhui yaliyomo ndani ya Katiba na kufanya maamuzi sahihi pindi siku ya kupiga kura itakapowadia. 

Aidha, mkakati huo wa kusambaza Katiba inayopendekezwa kwa njia ya sauti unajumuisha utoaji elimu kuhusu mfumo mpya wa kujiandikisha kwa njia ya kieletroniki (Biometric Voters Registration – BVR) pamoja na kuhamasisha wananchi ili wajitokeze kwa wingi kujiandikisha na kutimiza haki yao ya kikatiba wakati wa upigaji kura.

Akipokea, nakala za CD zenye Katiba inayopendekezwa kwa njia ya sauti, Mkurugenzi Mkaazi wa UNESCO nchini Tanzania Bi Zulmira Rodrigez, alipongeza Kampuni ya Focus Media kwa kuandaa matoleo hayo na kusisitiza radio za jamii kuzitumia ili kuwaelimisha wananchi mikoa yote juu ya Katiba inayopendekezwa.

 “Nimefurahi sana kuona hizi nyenzo za kisasa kama SD cards, kwa sababu tunaonesha kwamba radio za jamii ni njia bora zaidi za kutoa taarifa na pia zinawezesha kupata mrejesho kutoka kwa wananchi.”

Bi Zulmira Rodrigez, ameongeza kusema “Hili ni jambo zuri sana kwa jamii, na inapeleka taarifa mpaka katika njia ya chini kabisa, vijiji vilivyoko ndani kabisa.” 

Mwenyekiti wa mtandao wa redio za jamii Bwana Joseph Sekiku amewashuri watangazaji wa redio mbalimbali wliohudhuria semina hiyo amewaasa kutumia muda uliobai wa siku28 vizuri ili kuelimisha jamii maudhui ya Katiba inayopendekezwa ili wananchi wafanye maamuzi sahihi katika kura ya maoni na uchaguzi mkuu.

Sekiku ameongeza kwamba kwa sasa itapatikana kupia Focus Media pro ltd kwa kupitia mitandao yote ya kijamii na redio mtandao na wananchi wanaweza kuwasiliana kwa kutuma ujumbe mfupi kupitia namba +255 772 55 55 53
+255(0)772 55 55 53
LISTEN LIVE
http://myradiostream.com/25/8622
Tume ya Taifa Ya Uchaguzi Tanzania
YOUTUBE / TV
http://bitly.com/1Leujup
VIPINDI VYA REDIO
http://bitly.com/1Clt0r8 
FACEBOOK
http://bitly.com/1zIiIkq 
TWITTER
http://bit.ly/1678Vq2

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.