Balozi
wa Tanzania nchini China, Mh. Abdulrahman Shimbo (wa tatu kushoto) na mkewe
Mama Shimbo (wan ne kushoto), wakiwa na viongozi wa Jumuiya ya Wanafunzi
Watanzania Beijing (TZ-SUB) katika sherehe za miaka 51 ya Muungano wa
Tanganyika na Zanzibar (Tanzania) zilizofanyika Ubalozini mjini hapa. Mh Balozi
Shimbo alikuwa mgeni rasmi. (Picha na Fabian James)
Balozi
wa Tanzania nchini China, Mh Abdulrahman Shimbo akitoa mawaidha kwa waalikwa
katika sherehe za miaka 51 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar (Tanzania)
zilziofanyika Ubalozini mjini hapa. Mh Balozi Shimbo alikuwa mgeni rasmi katika
hafla hiyo iliyoandaliwa na Jumuiya ya Wanafunzi Watanzania Beijing
(TZ-SUB).(Picha na Salum Ramadhan)
Balozi
wa Tanzania nchini China, Mh. Abdulrahman Shimbo (wa pili kushoto) na mkewe (wa
tatu kushoto) katika picha ya pamoja na viongozi wa Jumuiya za Wanafunzi
Beijing kutoka nchi za Afrika Mashariki waliohudhuria sherehe za miaka 51 ya
Muungano wa Tanganyika na Zanzibar (Tanzania) zilizofanyika Ubalozini mjini
hapa. Balozi Shimbo alikuwa mgeni rasmi. (Picha na Salum
Wanafunzi
Wakitanzania Beijing pamoja na wageni mbalimbali katika picha ya pamoja na
mgeni rasmi, Balozi wa Tanzania nchini China, Abdurahman Shimbo (mwenye suti
katikati) na mkewe, katika sherehe za miaka 51 ya Muungano wa Tanganyika na
Zanzibar (Tanzania) zilizoandaliwa na Jumuiya ya Wanafunzi Beijing (TZ-SUB) na
kufanyika Ubalozini mjini hapa. (Picha na Fabian James)
Mwenyekiti
wa Jumuiya ya Wanafunzi Beijing (TZ-SUB), Ireneus Kagashe (kulia) akitoa
utangulizi katika sherehe za Muungano wa Tanganyika na Zanzibar (Tanzania)
zilizofanyika Ubalozini mjini hapa. Wa kwanza kushoto ni mgeni rasmi wa sherehe
hizo, Balozi wa Tanzania, China, Mh. Abdulrahman Shimbo, Mkewe Mama Shimbo na
Katibu wa Shirikisho la Jumuiya za Wanafunzi nchini China, Michael. (Picha na
Salum Ramadhan)
Familia
na Wafanyakazi wa Ubalozi wa Tanzania nchini China katika picha ya pamoja
wakati wa sherehe za miaka 51 ya Muungano zilizofanyika Ubalozini mjini hapa.
Sherehe hizo ziliandaliwa na Jumuiya ya Wanafunzi Watanzania Beijing (TZ-SUB).
Wa sita kutoka kushoto ni mgeni rasmi Balozi wa Tanzania nchini China, Mh.
Abdulrahman Shimbo, kushoto kwake ni mkewe, Mama Shimbo (Picha na Salum
Ramadhan)
No comments:
Post a Comment