Habari za Punde

Wachezaji wa Zamani wa Barcelona Wakutana na Rais Shein Ikulu Zanzibar

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Ikulu Mhe Dk Mwinyihaji Makame akisalimiana na Nyota wa timu ya Barcelona na Rais wa Heshima wa Timu hiyo Johan Cruyff, walipowasili Ikulu Zanzibar kusalimiana na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein, ni mwenyeji wao aliowaalika kutembelea Zanzibar kujionea vipaji vya wachezaji wa timu ndogo za Zanzibar.
Wachezaji Nyota wa Zamani wa Timu ya Barcelona wakisalimiana na Waziri Mwinyihaji walipowasili Ikulu Zanzibar kwa kusalimiana na Rais wa Zanzibar katika mualiko wa chakula cha mchana aliowaandalia wageni wake.
Waziri wa Habari Utamaduni Utalii na Michezo Zanzibar Mhe Said Ali Mbarouk akizungumza na mchezaji nyota wa timu ya Barcelona  Kulvert  wakati wa chakula cha mchana walioandaliwa na Rais wa Zanzibar Dk Shein Ikulu.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein, akizungumza  na Rais wa Heshima wa Timu ya Barcelona Johan Cruyff,  wakati wa chakula cha mchana aliowaandalia  wageni wake Ikulu Zanzibar, timu ya Barcelona ikiwa Zanzibar kwa mualiko wa Rais Shein.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein, akizungumza na ujumbe wa timu ya wachezaji wa zamani nyota wa Barcelona wakati wa chakula cha mchana aliowaandalia Ikulu, kulia Waziri wa Habari Utamaduni Utalii na Michezo Zanzibar Mhe Said Ali Mbarouk  na kushoto Kocha na Rais wa Heshima wa timu ya Barcelona Johan Cruyff.
Makamu Mwenyekiti wa Baraza la Taifa la Michezo Zanzibar Ndg Khamis Abdallah Said, akizungumza na kuutambulisha ujumbe wa Wachezaji wa Zamani wa timu ya Barcelona kwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Shein Ikulu Zanzibar wakati wa hafla ya chakula cha mchana.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein, akiwahutubia wachezaji nyota wa timu ya Barcelona wakati wa hafla ya chakula cha mchana  kilichofanyika Ikulu Zanzibar. Timu hiyo ikiwa Zanzibar kwa mwaliko wa Rais wa Zanzibar Dk Shein.
Wachezaji nyota wa Zamani wa timu ya Barcelona wakimsikiliza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein, wakati akizungumza na wachezaji hao walipofika Ikulu Zanzibar kuonana na mwenyeji wao Rais wa Zanzibar na kupata chakula cha mchana.
Wachezaji nyota wa Zamani wa timu ya Barcelona wakimsikiliza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein, wakati akizungumza na wachezaji hao walipofika Ikulu Zanzibar kuonana na mwenyeji wao Rais wa Zanzibar na kupata chakula cha mchana.
Mchezaji wa Zamani wa timu ya Barcelona na Rais wa Heshima wa timu ya Barcelona Johan Cruyff akizungumza wakati wa hafla hiyo wakati walipokutana na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein, Ikulu kwa chakula cha mchana walioandaliwa na mwenyeji wao.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein, akikabidhiwa jezi ya Timu ya Barcelona yenye jina la Cruyff namba 14. Iliokuwa ikivaliwa na mchezaji huo, akimkabidhi jezi hiyo Rais wa Heshima wa Timu ya Barcelona Johan Cruyff,  wakati wa hafla ya chakula cha mchana kilichofanyika Ikulu Zanzibar.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein, akikabidhiwa jezi ya Timu ya Barcelona yenye jina la Cruyff namba 14. Iliokuwa ikivaliwa na mchezaji huo, akimkabidhi jezi hiyo Rais wa Heshima wa Timu ya Barcelona Johan Cruyff,  wakati wa hafla ya chakula cha mchana kilichofanyika Ikulu Zanzibar.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein, akimkabidhi zawadi ya kitabu cha historia ya Utalii wa Zanzibar Rais wa Heshima wa Barcelona Johan Cruyff. Wakati wa hfla ya chakula cha mchana aliowaandaliwa wachezaji hao Ikulu Zanzibar.    
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein, akimkabidhi zawadi ya Karafuu akitowa maelezo ya karafuu hiyo kwa  Rais wa Heshima wa Barcelona Johan Cruyff. Wakati wa hafla ya chakula cha mchana aliowaandaliwa wachezaji hao Ikulu Zanzibar.   
Wajumbe wa Kamati ya matayarisho ya mapokezi ya Timu ya Wachezaji wa Zamani wa Barcelona wakiwa katika hafla hiyo wakimsikiliza Rais wa Zanzibar Dk Shein, akizungumza na wachezaji hao walipofika Ikulu.
Wajumbe wa Kamati ya matayarisho ya ugeni wa timu ya Barcelona wakiwa katika ukumbi wa  hafla hiyo wakifuatilia mazungumzo ya Rais wa Zanzibar na wachezaji hao.wakwanza Katibu Mkuu Wizara ya Habari Utamaduni Utalii na Michezo Zanzibar Ndg  Ali Mwinyikai.
Wachezaji wa timu ya Taifa ya Zanzibar wakiwa katika hafla hiyo kujumuika na wachezaji wa zamani wa Barcelona Kocha Gulam alikuwa mchezaji wa timu ya Taifa na timu ya miembeni na Omar Yussuf Chunda nae alikuwa mchezaji wa timu ya Taifa ya Zanzibar na mchezaji wa timu ya miembeni Zanzibar.
 











No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.