BAADHI ya watendaji wa kituo cha huduma za
sheria Zanzibar ZLSC, wakifuatilia hutuba iliotolewa na rais wa mahakama ya
Afrika ya haki za binadamu na haki za watu, jaji Agostino Ramadhan alioitoa
kwenye mahafali ya tatu ya wasaidizi wa sheria wa majimbo ya Ugunja na Pemba,
yaliofanyika ZSSF mjini Chake chake Pemba, (Picha
na Haji Nassor, Pemba).
MKURUGENZI mtendaji wa kituo cha huduma za sheria Zanzibar
ZSLC, Harusi Miraji Mpatani, akielezea dhana ya wasaidizi wa sheria ilivyozaa
matunda, ambayo ilianzishwa na kituo hicho tokea mwaka 2007, kwenye mahafali
yao ya tatu yaliofanyika ZSSF mjini Chake chake Pemba, (Picha na Haji Nassor, Pemba).
WASANII wa ngoma ya kibati ‘MKOTA
NGOMA’kutoka wilaya ya Mkoani, wakitikisha jukwaa kwa kupamba mahafali
ya tatu ya wasaidizi wa sheria wa majimbo ya yote ya Zanzibar, yaliofanyika
Chake chake Pemba, (Picha na Haji
Nassor, Pemba).
WAANDISHI wa habari wa vyombo mbali mbali,
wakiwa kazini kwenye mahafali ya tatu ya wasaidizi wa sheria wa majimbo 52 ya
uchaguzi, wasaidizi hao wamesomeshwa na kituo cha huduma za sheria Zanzibar
ZLSC kwa muda wa miaka miwili, (Picha na
Haji Nassor, Pemba).
MWENYEKITI wa bodi ya wadhamini wa
kituo cha huduma za sheria Zanzibar ZLSC, Pro: Chris Maina Peter akielezea
namna kituo hicho kinavyofanya kazi ya kutoa msaada wa sheria kwa jamii ya
wazanzibari, kwenye mahafali ya tatu ya wasaidizi wa sheria yaliofanyika mjini
Chake Chake Pemba, (Picha na Haji
Nassor, Pemba).
RAIS wa mahakama ya Afrika ya haki za
binadamu na haki za watu, jaji Agostino Ramadhan, akiwahutubia wasaidizi wa
sheria 68 waliohitimu mafunzo yao ya miaka miwili, kwenye mahafali yao ya tatu
ualiofanyika ZSSF mjini Chake chake Pemba, (Picha
na Haji Nassor, Pemba).
RAIS wa mahakama ya Afrika ya haki za
binadamu na haki za watu, jaji Agostino Ramadhan, akimkabidhi cheti mmoja wa
wasaidizi wa sheria kati ya 68, kutoka majimbo 52 ya uchaguzi ya Zanzibar,
hafla hiyo ilifanyika mjini Chake chake kisiwani Pemba, (picha na Haji Nassor, Pemba).
RAIS wa mahakama ya Afrika ya haki za
binadamu na haki za watu, jaji Agostino Ramadhan akionyesha zawadi maalumu
aliokabidhiwa na uongozi wa kituo cha huduma za sheria Zanzibar , kwenye
mahafali ya tatu ya wasaidizi wa sheria, yaliofanyika mjini Chake chake Pemba, (Picha na Haji Nassor, Pemba).
AFISA mipango wa kituo cha huduma za
sheria Zanzibar ZLSC tawi la Pemba, Safia Saleh Sultan akijubu hoja za
washiriki wa kongamano, lililofuatiwa na hafla ya kuwatunuku vyeti , kongamano hilo lilifanyika mjini Chake chake
Pemba, (Picha na Haji Nassor, Pemba).
No comments:
Post a Comment