Na Hassan Khamis, Pemba
MAHAKAMA ya mwanzo Wete, imetoa
hukumu ya kifungo cha miezi miwili kutumikia chuo cha Mafunzo, kwa mshtakiwa
Luhasa Ndengule Kashere (20) mkaazi wa Junguni Gando, aliyedaiwa kuiba jembe
moja.
Mara
baada mshtakiwa kupanda kizimbani akisubiri taratibu za mahakama, ndipo hakimu
wa mahakama hiyo Abubakar Suleiman Thabit alipotoa hukumu hiyo kwa mshatikiwa.
“Mshtaliwa,
kwa vile ni kosa lako la mwanzo na hatuna kumbukumbu ya makosa uliyofanya
nyuma, adhabu yako kutokana na kosa hili ni miezi mitatu lakini nakufanyia
tahfifu, utatumikia chuo cha mafunzo kwa muda wa miezi miwili”, alisema Hakimu
huyo.
Hakimu
huyo amesema kilimo ni uti wa mgongo wa taifa hivyo kitendo cha kuiba jembe ni
sawa na kuvunja uti huo wa mgongo hivyo mahakama imejiridhisha na maelezo
yalitolewa na mashahidi wa pande zote mbili.
Mwendesha
mashtaka wa Polisi stesheni sajenti Khamis Faki Simai alidai mahakani hapo kuwa
April 5, mwaka huu baina ya saa 4:00 asubuhi na saa 8:00 mchana, bonde la bibi
Wangoji Junguni Gando Wete Mshtakiwa alliba jembe moja la kulimia lenye thamani
ya shilingi 6000 mali ya Thani Juma Hamad.
Kufanya
hivyo ni kosa kinyume na vifungu 267 (1) na 274 (1) vya kanuni ya adhabu sheria
namba 6 ya mwaka 2004, sheria ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.
No comments:
Post a Comment