Mratibu wa Jumuiya ya Maradhi Yasioambukiza Zanzibar Ndg, Omar Abdalla akizungumzia maradhi ya Sukari kwa wananchi waliofika katika Tamasha la Kupambana na Ugonjwa wa Sukari Zanzibar lililoandaliwa na Shirika lisilo kuwa la Kiserikali la Uingereza la VSO na ISC, Ili kutowa elimu ya kupambana na ugonjwa wa sukari zanzibar.
Afisa wa Mradi wa Vijana Waliojitolewa wa Shirika la VSO - ICS Ndg Franklin Kebelo, akizungumza wakati wa Tamasha la Pambana na Ugonjwa wa Kisukari kwa kula Matunda na Mbogamboga, ili kuepusha kupata Sukari. lililofanyika katika viwanja vya mpira vya malindi Zanzibar.
Baadhi ya Vijana kutoka Uingereza na Tanzania waliojitolea wa katika Shirika la VSO na ISC, kuwahamasisha wakulima wa matunda na mbogamboga kuimarisha kilimo hicho, wakiwa katika viwanja vyac mpira malindi Zanzibar wakishiriki katika tamasha hilo na kutowa elimu kuhusiana na kukabiliana na ugonjwa wa sukari kwa kutowa ushauri kwa wananchi waliofika katika tamasha hilo.
Wananchi wa Zanzibar wakijitokea kupia afya zao kwa kucheki Sukari na kupima Presha huduma hiyo imetolewa na kwa ushirikiano wa Madaktari wa Magonjwa Yasioambukiza Zanzibar kwa kutowa huduma ya vipimo vya Sukari na Presha.
Daktari kutoka Jumuiya ya Maradhi Yasioambukiza Zanzibar akimpima mmoja wa Wananchi waliofika katika Tamasha hilo kupima afya yake.
Daktari kutoka Jumuiya ya Maradhi Yasioambukiza Zanzibar akimpima Sukari mmoja wa Mwananchi aliyefika katika Tamasha hilo katika viwanja vya malindi Zanzibar.
Wanachi waliofika katika viwanja va mpira malindi katika Tamasha la Kupambana na Ugonjwa wa Sukari Zanzibar wakisubiri kupima Presha na Sukari. Huduma hiyo imetolewa bure na Shirika la VSO na ISC kwa kushirikiana na Madaktari wa Maginjwa Yasioambukiza Zanzibar.
Kijina wa VSO na ISC Ndg Suleiman Bakari akitowa maelezo ya Matunda yanayposwa kutumiwa na mgonjwa wa Sukari, wakati wa tamasha hilo lililofanyika katika viwanja vya mpira vya malindi Zanzibar.
Vijana wa Kujitolea wa VSO na ISC kutokwa Uingereza wakichezesha mchezo jinsi ya matumizi ya matunda yanayofaa kutumiwa na mgonjwa wa sukari wakati wa Tamasha hilo lililofanyika katika viwanja vya mpira malindi Zanzibar.
Jijana wa VSOna ISC kutoka Tanzania Bi Stella John, akitowa maelezo kwa wananchi waliofika katika Tamasha hili jinsi ya matumizi ya viwanja kwa binaadamu jinsi sukari iliyomo katika viwanja hivyo kama anavyoonesha moja ya kinywaji hicho jinsi ya sukari iliyomo. na kutowa ushauri kupigunza kunywa kinyaji bari kwa wingi ndio unavyojiongezea sukari mwili.
Kikundi cha Mazoezi cha Obama Zanzibar kikitowa mazoezi wakati wa Tamasha hilo la Kupambana na Ugonjwa wa Kisukari kwa kula Mbogamboga na Matunda na kufanya mazoezi.
No comments:
Post a Comment