Habari za Punde

Jumuiya ya Vijana Wasio na Ajira Tanzania Yazinduliwa Rasmin Zanzibar.

Muongozaji wa Mkutano wa Uzinduzi wa Jumuiya ya Vijana wasio na ajira Tanzania TUEPO Msabah Ali Msabah akitoa maelezoa kwa washiriki wa Mkutano huo uliofanyika Ukumbi wa Water Front Rahaleo Mjini Zanzibar.
Mwenyekiti wa TUEPO Ussi Said Suleiman akimtoa maelezo mafupi ya Jumuiya hiyo na kumkaribisha mgeni rasmi kufungua mkutano huo.
Mgeni rasmi Katibu Mtendaji Baraza la Vijana Zanzibar Khamis Faraji Abdalla akizindua Jumuiya ya watanzania wasio na ajira (TUEPO)  katika Ukumbi wa Water Front Rahaleo Mjini Zanzibar. Picha na Makame Mshenga-Maelezo Zanzibar. 
Viiongozi wa Jumuiya ya TUEPO wakiwa katika picha ya pamoja na Katibu Mtendaji Baraza la Vijana  Zanzibar (suti nyeusi)  baada ya kufungua mkutano huo. Picha na Makame Mshenga-Maelezo Zanzibar.

Mwenyekiti wa TUEPO Ussi Said Suleiman akiagana na Katibu Mtendaji Baraza la Vijana Zanzibar Khamis Faraji Abdalla.
Na Maryam  Kidiko / Rahma Khamis  Maelezo.                                                          
Katibu Mtendaji Baraza la Vijana Zanzibar Nd. Khamis  Faraji Abdallah amewataka Vijana kujiunga  katika Taasisi zitakazo wawezesha kuwainuwa kimaisha.

Hayo ameeleza katika Ukumbi wa Water front  Raha leo wakati alipokuwa akizindua Jumuiya  ya vijana wasio na ajira Tanzania  (Tanzania unemployed people organization) TUEPO .

Amesema Baraza la Vijana Zanzibar lipo kwa ajili ya kuwasikiliza na kuwaelekeza vijana  ambao hawana ajira ili waweze kujiendeleza na kujiimarisha katika shughuli  mbali mbali za maendeleo ili  waweze kujiari  wenyewe .


“ Ni lazima tufanye kazi kwa pamoja ili Baraza la Vijana Zanzibar  liweze kuimarika na kufanyakazi  kwa ufanisi,”  aliesema Katibu  Khamis.

Akizungumzia   lengo la Baraza hilo amesema  ni kuwawakilisha Vijana   kufaidika na fursa zilizopo,  kuwawezesha   kujielewa,  pamoja na kuwashajiihisha kuwa na uwezo wa kuzalisha mali.

“Ni vizuri kushirikiana  pamoja ili vijana waweze kuimarika katika maisha yao na Jamii kwa ujumla,” amesisitiza Khamis Faraji.

Katibu huyo amewapongeza wanajumuiya hao kwa kufanikisha kuanzisha taaluma mbali mbali  ikiwemo  Ubaharia, Udereva, ushoni, Mapishi pamoja na kusomesha lugha ya kiengereza ambayo lengo lake ni kuwawezesha  vijana  kuajirika katika  Hoteli mbalimbali za  ndani na nje ya nchi.

“Tutumie fursa iliyopo kwa ufanisi  zaidi bila ya kujali itikadi   ya vyama vya  siasa,”  ameongeza Khamis  Faraji.

Nae Mwenyekiti wa Jumuiya  ya TUEPO  Ussi Saidi Suleiman  amesema wanatarajia  kuwapatia mafunzo ya ubaharia vijana watatu,  vijana 15  mafunzo ya mapishi, kumi  ushoni na vijana 20  wanatarajiwa kusomeshwa lugha ya kiengereza.

Mwenyekiti huyo ameiomba Serikali kuwapatia mikopo ambayo itawawezesha vijana kuwaendeleza katika kukuzi vipaji na kujiendeleza kiuchumi sambamba na kuanzishwa viwanda ili vijana  waweze kupata ajira.

Jumuiya hiyo  imeanzishwa  mwezi uliopita  na  ina wanachama 73 hadi hivi sasa.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.