Habari za Punde

Kituo cha Sheria Pemba Chatowa Mafunzo kwa Askari.

 Mratibu wa Kituo cha Huduma za Sheria Zanzibar ZLSC Tawi la Pemba Bi.Fatma Hemed Khamis akizungumzia kazi na majukumu ya Kituo hicho, kwenye mafunzo kuwatambaulisha wasaidizi wa Sharia kwa Watendaji wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Kaskazini Pemba, kulia ni Afisa Mipango wa Kituo Bi.Safia Saleh Sultan na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kaskazini Pemba Mohamed Sheikhan Mahamed, mafunzo yaliofanyika kituoni hapo.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kaskazini Pemba Mohamed Sheikhan Mohamed akifungua mafunzo ya siku mbili watendaji wa Jeshi lake la Mkoa huo kuhusu kuwatambulisha wasaidizi wa sharia, mafunzo yalioandaliwa na Kituo cha Huduma za Sheria Zanzibar ZLSC tawi la Pemba wa mwanzo kulia ni afisa mipango wa Kituo  Safia Salhe Sultan, akifuatiwa na Mratibu wake Fatma Hemed Khamis na kushoto ni mtoa mada pia hakimu wa mahakama ya wilaya ya Chake chake Omar Mcha Hamza
 Watendaji wa Jeshi la Polisi mkoa wa kaskazini Pemba wakiimba wimbo maamlumu wa maadili kabla ya Kamanda wa Polisi mkoani humo  Mohamed Sheikhan Mohamed, kufungua mafunzo ya siku mbili ya kuwatambulisha wasaidizi wa sharia, yalioandaliwa na Kituo cha Huduma za Sheria Zanzibar ZLSC, (Picha na Haji Nassor, Pemba).

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.