Habari za Punde

ZSSF Yatoa Elimu Kwa Maofisa Utumishi Juu ya Mafao ya Uzazi kwa Wafanyakazi

                                             
Ofisa Uhusiano wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii Zanzibar (ZSSF) Ndg. Mussa Yussuf, akitowa maelezo kwa Maofisa Utumishi kabla ya kuaza kwa Mkutano huo wa kutowa Elimu juu ya Mafao ya Uzazi.   
Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Mhe Abdalla Mwinyi Khamis, akifungua mkutano wa Maofisa Utumishi wa Serikali na Taasisi za Umma na Binafsi kuhusiana na Mafao ya Uzazi kwa Watumishi Wanachama wa ZSSF.uliofanyika katika ukumbi wa kiwanja cha watoto kariakoo Zanzibar.
Mkurugenzi Muendeshaji wa Mfuko wa Jamii Zanzibar (ZSSF) Ndg. Abdulwakil Haji Hafidh, akitowa maelezo ya Utendaji wa ZSSF kwa Maofisa wa Utumishi,wakati wa semina ya siku moja ya kutowa Elimu kwa Maofisa Utumishi wa Taasisi za Serikali na Binafsi Zanzibar, semina hiyo imefanyika katika ukumbi wa Uwanja wa Wawtoto Kariakoo Zanzibar.
            Maofisa Utumishi na Uendeshaji wakifuatilia Semina hiyo wakati wa kuwasilishwa mada.
Meneja wa Mipango Utafiti na Uwekezaji ZSSF, Ndg. Khalifa Muumin, akitowa Mada kuhusiana na chimbuko la Mafao ya Uzazi kwa Washiriki wa Semina hiyo iliowashirikisha Maofisa Utumishi na Uendeshaji katika Taasisi za Serikali na Taasisi za Binafsi Zanzibar, Akitowa Elimu hiyo kwa Washiri katika ukumbi wa Kiwanja cha Kufurahishia Watoto Kariakoo Zanzibar 

Afisa wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii Zanzibar Bi. Zainab Rajab, akitowa Mada kuhusiana na Mafao ya Uzazi kwa Wanasemina,na kutoa Ufafaninuzi wa Jinsi ya Malipo ya Mafao ya Uzazi kwa Wananchama wa ZSSF Zanzibar.

Mwanasheria wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii Zanzibar Ndg. Mohammed Faki, akitowa Mada kuhusiana Sheria kwa Mwanachama wa ZSSF jinsi ya kupata Mafao yake baada ya kustaafu. na kutowa maelezo vipi Mwanachama anweza kupata mafao yake kisheria.  
Maofisa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii Zanzibar ZSSF wakimsikiliza Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi akifungua Mkutano wa Maofisa Utumishi wa Wizara za Serikali na Mashirika ya Umma na Taasisi Binafsi kuhusiana na Mafao ya Uzazi.
Maofisa Utumishi wakiwa katika Ukumbi wa Mkutano wakisikiliza Mada zilizokuwa zikiwakilishwa wakati wa Mkutano huo wa kutowa Elimu Juu ya Mafao ya Uzazi na Kuchangia kwa hiari. uliofanyika katika ukumbi wa kiwanja cha Watoto Kariakoo Zanzibar. 
Maofisa Utumishi wa Wizara za Serikali na Mashirika ya Umma na Taasisi Binafsi wakiwa katika ukumbi wa Mkutona wakifuatilia mada mbalimbali zinazowakilishwa na Maofisa wa ZSSF kuhusiana na Mafao kwa Wanachama wake, Mkutano huo umefanyika katika Ukumbi wa Kiwanja cha Watoto Kariakoo Zanzibar.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.