Habari za Punde

BLW kuanza kikao chake cha 20 Mei 13


 Na Ali Issa-Maelezo Zanzibar, 11/5/2015.

Mkutano wa Ishirini wa Baraza la Nane la Wawakilishi la Zanzibar unatarajiwa kuanza Siku ya Jumatano ya Mei 13, mwaka huu katika Ukumbi wa Baraza hilo Mbweni nje kidogo ya mji wa Zanzibar.

Katika Mkutano huo kutakuwa na Majadiliano ya Bajeti ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kwa mwaka 2015/2016.

Akitoa Muhutasari wa Mkutano huo leo Katibu wa Baraza la Wawakilishi Yahya Khamis Hamad amesema Wajumbe wa Baraza hilo watapata nafasi pana ya kujadili Bajeti hiyo ambayo ndio mwelekeo mzima wa Shughuli zote za kiserikali.

Amesema frusa  hiyo nimuhimu kwa Wajumbe hao kuitumia vyema kujadili mambo ya msingi yanayowahusu Wananchi wao badala ya kujadili mambo ambayo hayatakuwa na faida kwao.

Aidha Katibu huyo amewashauri Wananchi wa Zanzibar kushirikiana na wakilishi wao na kujadili masuala yenye kipau mbele nao ili kutatua changamoto zinazo wakabili katika Majimbo yao.

Katibu Yahya amesema Miswaada Miwili ya Sheria itawasilishwa na  kujadiliwa ikiwemo mswada wa Sheria ya Fedha na Mswada wa Sheria wa kuidhinisha matumizi ya Serikali kwa mwaka 2015/2016

Aidha amefahamisha kuwa Jumla ya Maswali 81 yataulizwa na kujibiwa katika Mkutano huo.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.