Katibu wa Baraza la Wawakilisahi Zanzibar Mhe Yahya Khamis Hamad, akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na ratiba ya Kikao cha Baraza la Wawakilishi cha Bajeti ya mwaka 2015/-2016, linalotarajiwa kuaza kesho katika ukumbi huo na kuwasilishwa Miswada na Maswali 81 yatakayoulizwa katika Kikao hicho.
Katibu wa Baraza la Wawakilishi Mhe Yahya Khamis Hamad, akizungumza na waandishi wa habari wa vyombo mbalimbali vilioko Zanzibar kuhusiana na kuaza kwa Mkutano wa Ishirini wa Baraza la Nane la Wawakilishi Zanzibar, Amesema katika mkutano huo wa Baraza utakuwa na kuwasilishwa kwa Maswali 81 na Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi na kuwasilishwa Bajeti ya Serikali kwa mwaka 2015-2016. Pia amesema katika Mkutano huo kutawasilishwa Miswada wa Sheria miwili itawasilishwa na kujadiliwa katika kikao hichoMiswada ya Sheria
1. Mswada wa Sheria ya Fedha (Finance Bill)
2. Mswada wa Sheria ya Kuidhinisha Matumizi ya Serikali kwa Mwaka 2015-2016 (Appropriation Bill)
Waandishi wa habari wa vyombo mbali mbali wakifuatilia mkutano na Katibu wa Baraza wakati akitoa taarifa ya kukamilika kwa Kikao cha Bajeti kinachotarajiwa kufanyika kesho na kuwakilishwa Bajeti ya Serikali Zanzibar.
Waandishi wakifuatilia mkutano huo, uliofanyika katika Ofisi za Baraza la Wawakilishi ukumbi mdogo.
No comments:
Post a Comment