Habari za Punde

Serikali kuzipatia maeneo mengine Afisi za Tume ya Uchaguzi za wilaya

Na Miza Othman / Rahma Khamis- Maelezo Zanzibar    

Serikali inampango wa kuzipatia maeneo mengine Afisi  za Tume ya Uchaguzi za Wilaya zilizopo karibu na Afisi za Wakuu wa Wilaya pindi hali ya kifedha itakaporuhusu na Waheshimiwa wajumbe wavute subra kwa ajili ya ujenzi ya Afisi hizo

Hayo yameelezwa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamo wa Pili wa Rais Balozi Seif Ali Iddi leo huko katika Ukumbi waBaraza la Wawakilishi Chukwani nje kidogo ya Mji wa Zanzibar wakati akijibu suali la Mh.Salleh Nassoro Juma (Jimbo la Wawi) wakati alipotaka kujuwa  Sababu  za kuhamishwa Afisi za Tume ya Uchaguzi za Wilaya.

Amesema  kuwepo kwa Afisi hizo hakuvunji Demokrasia wala misingi ya Utawala bora kutokana na sababu za msingi zinazopelekea baadhi ya Afisi za Tume kufanya kazi zake ubavuni mwa wakuu wa Wilaya  ni upungufu wa maeneo husika.

Waziri huyo amesema kuwepokwa Afisi za Tume hizo Karibu na Ofisi za Wakuu hao haimainishi kuwa watendaji wa Tume wanafanya kazi kwa maelekezo ya Wakuu hao kama inavyobuniwa na baadhi ya wanasiasa.


Aidha amesema kwakuwa kazi hizo zililazimika kufanyika kabla ya uchaguzi Mkuu wa mwaka 2005 Tume iliomba kupatiwa Ofisi katika kila Wilaya kutokana na maombi hayo Ofisi za Wakuu wa Wilaya ziliipatia Tume hiyo kwa muda ili kuendesha kazi zake.

Hata hivyo akifafanuwa kuhusu Afisi hizo amesema kwamba  kwa upande wa Pemba Afisi tatu kati ya nne ziko ubavuni mwa majengo ya Wakuu wa Wilaya na kwa Unguja Asifi mbili kati ya sita zipoubavuni kwa Wakuu hao.

Sambamba na  hayo  kwa mujibu wa masharti ya Sheria ya Uchaguzi wa Zanzibar ya mwaka 1984 katika kutetekeleza ilifanyiwa marekebisho kwa kopitia sheria no. 12 ya 2002 ilianzisha Daftari la kudmu la Wapiga kura ili kazi zao zifanyike kwa ufanisi.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.