Na Miza Othman / Rahma Khamis- Maelezo
Serikali imetakiwa na Wananchi wa Kijij cha Tumbe kujenga soko la kisasa ili kuweza kuendeleza kufanya biashara zao kwa ufanisi na kuepukana usumbufu usio wa lazima.
Hayo yamesemwa na Waziri wa Mifugo na Uvuvi Abdilah Jihad Hassni leo huko Baraza la wawakilishi Chukwani nje kidogo ya Mjiwa Zanzibar wakati akijibu sualila la Mwakilishi wa Jmbo la Wawi Saleh Nassor Juma
Kutaka kujuwa Sababu zilizopelekea kulazimishwa wavuvi warejee kuuza samaki wao katika soko la Tumbe wameshaachana nalo kwa muda mrefu.
Amesema Serikali inawajibu wa kuwataka Wavuvi hao waondoe tofauti zao na kurudi kutumia miundombinu iliyogharimu Miliono mia saba za mkopo wa uhisani wa Benki ya dunia kutumika ipasavyo.
Waziri Abdilah Jihad amesema Wizara yake kupitia mradi huo ulifanikisha kuanza ujenzi wa soko ndani ya mwaka 2011 na kumalizika mwaka 2014 itapelekea kutofahamiana baina ya wenyeji wa Tumbe na maeneo mengine wanaoleta samaki hao.
Aidha ameeleza kuwa kutokana na hali hiyo wavuvi wamaeneo mengine wanaoleta samaki wao katika diko hilo wametakiwa wasivue samaki kwa mfumo wa kuzamia chini ya Bahari katika mwezi wa Ramadhani kwani uzamiaji huo hupelekea wavuvi hao kutokuwa na funga ,wanapouza samaki wao madhambi yao yanakwenda kwa wananchi wa kijiji hicho.
Hata hivyo wananchi wametakiwa kuondowa tofauti zao na kulitumia soko hilo vizuri ili kuljitea maendelo ndani ya biashara zao.
No comments:
Post a Comment