Na Haji Nassor, Pemba
HARAKATI za kuelekeza uchaguzi mkuu tayari zimeanza kupamba moto kwenye vyama vya siasa na wapo waliokwisha tangaaza nia, wakianza kuwindana majimboni.
Bila shaka wagombea hawa, mbeleko wao tayari wameshaelekeza jicho kuvitumia vyombo vya habari wapendavyo na hasa baada ya kumrambisha mwandishi visenti.
Wapo wgombea ambao wameshatangaaza nia na wameshajipangia bajeti zao, kwamba kiasi fulani zitakwenda wa wapambe, wenyeviti wa matawi na nyengine kwa waandishi wa habari.
Tumeshaanza kushuhudia baadhi ya waandishi wa habari wakianza kuwapigia kampeni kama sio debe wagombea na kufanywa mbeleko kwa kuandikwa na kutangaza nia.
Vyombo vya habari kamwe visikubali kufanywa mbelekeo kwa wagombea, kwani kufanya hivyo ni kukiuka maadili ya kazi zenu.
Mbona sasa vipo vyombo vya habari vimeanza kubeza, kudharau na kuponda wanachama waliotangaaza nia na kuwapamba wengine, je hili ni sahihi.
Lazima vyombo vya habari virudi kwenye maadili ya kazi zao ikiwemo ya “fairness’’ kwa maana ya kupunguza madhara kwa wengine, sasa iwapo chombo cha habari kitaegemea upande mmoja na kuacha mwengine, hapo kazi ya habari tunasema imeota mbawa.
Iweje chombo cha habari ambacho kintegemewa na wananchi wote wa taifa hili, kisha kianze kupiga mdongo chama kimoja na chengine kukipa hadhi?
Tena kwa mfano tume za uchaguzi zote mbili za Tanzania, hujitahidi kukaa na waandishi wa habari ili kuwakumbusha maadili yao, lakini vipo vyombo ambavyo wakati kama huu huweka mbele bahasha na kusahau maadili.
Wapo wataalamu wa habari waliosema kwamba, mwandishi au chombo cha habari kilichoshindwa kufauata maadili basi ni vyema kikajiondoa kuliko kufanywa mbeleko.
Kwa siku kama hizi kuelekea uchaguzi mkuu, wapo wagombea ambao watajenga ukaribu mno na waandishi wa habari na kujipendekeza sana, kumbe wanafauta mbeleko.
Katika hili, wagombea wanaweza kujifanya kama waliokosa bahati ndani ya jamii na kuwapa hadhi kubwa waandishi wa habari, hata kuitwa muheshimiwa.
Yote kwa yote waandishi wa habari na vyombo vyao, lazima wawemakini kwenye miezi hii ya kuelekea uchaguzi mkuu, maana wagombea wanaamini habari wazitakazo wao zikichapishwa ndio furaha yao.
Hiana maana kwamba habari za wagombea zisiandikwe au kutangaazwa kwenye vyombo vya habari la hasha, illa ni vyema kuhakikisha maadili na sheria zainaendelea kufuatwa.
Kwani hatukumbuki kwamba tathimini ya uchaguzi uliopita kwenye vyombo bvya habari, waandishi walivigawa vyama kwa kuviita vyengine vidogo?
Kama hivyo ndivyo, lazima waandishi wakiwa karibu na wahariri wao wahakikishe kwamba habari ambazo zitaletwa mbele yao, hazimvui nguo mgombea mwengine na kumvisha wa upande mwengine.
Lakini na nyinyi ambao mmeshatangaaza nia, sio busara kuwalazimisha waandishi kukiuka maadili kwa kuandika habari ambazo zinampaka matope mgombea mwenzako.
Kwa hili hata wadau wa vyombo vya habari lazima kwa nafasi yenu muhakikisha vyombo vya habari ambavyo vinapuuzia maadili yao musiviunge mkono.
No comments:
Post a Comment