Afisa Mkuu wa uwakilishi wa Kudumu wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa, Bw. Songelael Shilla, akizungumza wakati wa Mkutano wa pembezoni ( Side-Event) ulioandaliwa kwa ushirikiano kati ya Uwakilishi na Asasi za Kimataifa, kwaajili ya kubadilishana mawazo kuhusu nafasi za Ki Kanda na Kitaifa katika mfumo wa ufuatiliaji na udhibiti, fursa na changamoto za Malengo ya Maendeleo Endelevu baada ya 2015 kwa upande wa Afrika.
Sehemu ya Washiriki wa mkutano huo wa pembezoni ambapo washiriki pamoja na mambo mengine walisisitiza haja na umuhimu wa wananchi kushirikishwa kikamilifu katika eneo hilo la ufanyaji wa tathmini na ufuatiliaji kwa kile walichosema malengo hayo ya maendeleo endelevu yanawahusu wananchi hiyo ushiriki wako ni muhimu
Sehemu ya Sehemu wa Washiriki wa mkutano huo wa pembezoni ambapo washiriki pamoja na mambo mengine walisisitiza haja na umuhimu wa wananchi kushirikishwa kikamilifu katika eneo hilo la ufanyaji wa tathmini na ufuatiliaji kwa kile walichosema malengo hayo ya maendeleo endelevu yanawahusu wananchi hiyo ushiriki wako ni muhimu
Na Mwandishi Maalum, New York
Mchakato wa
ukamilishaji wa Malengo Mapya ya
Maendeleo endelevu baada ya 2015 ( SDGs)
umeingia katika hatua nyingine muhimu ambapo, nchi wanachama wa Umoja wa Mataifa
wanakutana hapa makao makuu ya UM wakijadiliana kuhusu mfumo wa
ufuatiliaji na tathmini ya
malengo hayo.
Mkutano huo unaojadili aina ya mfumo wa ufuatiliaji na
tathmini, utafanyika kwa siku nne na
umeanza siku ya jumatatu kwa wajumbe
kutoa mchango wa maoni na
mawazo yao kwa kuzingatia rasimu
iliyowasilishwa na wenyeviti- wenza wa mchakato wa majadiliano juu ya ajenda na malengo ya maendeleoe
endelevu baada ya 2015.
Karibu wajumbe wote waliozungumza katika siku
ya kwanza ya majadiliano haya, wametoa mapendekezo yao
yanayotaka mfumo huo wa ufuatiliaji na tathmini uwe wa nama
gani.
Akizungumza kwa
niaba ya Kundi la Nchi 77 na China (
G77&China) Mwakilishi wa Afrika ya
Kusini amesema nchi zinazounda kundi
hilo wangependa kuona kwamba mambo
yafuatayo pamoja na mengine mengi yanazingatiwa katika eneo hilo la
ufuatiliaji na tathmini.
Baadhi ya mapendekezo ya G77na China
ni mfumo wa ufuatiliani na tathimin uwe na upeo mpana na umilikiwe na nchi husika kwa kuzingatia mazingira yake, mahitaji yake na
vipaumbele vyake.
Kundi hilo limetaka
pia ufuatiliaji na tathmini, eneo ambalo ni muhimu katika utekelezaji
wa SDGs lazima uongozwe na kusimamiwa na
serikali na uwe wa hiari uzishikisha Wizara mbalimbali
na
wadau wengine ambao wataonekana kuwa ni muhimu.
Vile vile kundi la G77
na China limesisitiza haja na umuhimu wa
kuhakikisha kuwa mfumo wa ufuatiliaji na tathmini unapaswa uwe ujumuishi na wenye uwiano ukizingatia pia ajenda namba 17 na malengo
yote 169.
Kundi hilo la 77 na
China pia limeleza kwamba ni kwa kupitia mfumo wa ufuatiliaji na tathmini ndipo ambapo Umoja wa Mataifa utakuwa katika
nafasi nzuri kutathmini utekelezaji wa ajenda za maendeleo baada ya 2015
ili kuhakikisha kwamba lengo kuu la
malengo hayo ambalo ni kuondoka umaskini linafikiwa.
Wachangiaji wengine
wamesisitiza umuhimu wa uwazi,
ushirikishwaji na uwajibikaji wa makundi yote zikiwamo Taasisi
na mashirika ya Umoja wa Mataifa.
Baadhi ya
wazugumzaji wameeleza umuhimu wa matumizi sahihi ya takwimu, uwezeshwaji katika ukusanyaji wa takwimu hizo
ikiwa ni pamoja na umuhimu wa ushiriki wa Asasi zisizo za kiserikali katika mchakato huo wa ufuatiliaji na tathmini.
Wachangiaji wengine
wamekwenda mbali zaidi kwa kutaka ushiriki na ujumuishi wa wananchi katika eneo hilo kwa kile wanachosema ili utekelezaji wa malengo hayo uwe wenye tija wananchi wanapashwa kuwa sehemu
ya kufanya tathmini na kufuatilia kwa kuwa eneo kubwa la SDGs linahusu wananchi.
Jamhuri ya Muungano
wa Tanzania inashiriki kikamilifu katika
majadiliano yote muhimu ya
mchakato mzima maandalizi ya SDGs ambapo wawakilishi wa kutoka Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Tume ya Mipango Tanzania Bara na Visiwani na
Wawakilishi kutoka Asasi zisizo
za Kiserikali wamekuwa wakihudhuria
mijadala hiyo ikiwa ni pamoja na kusimamia maslahi ya Tanzania na
Bara la Afrika katika ujumla wake.
Aidha Tanzania
Kupitia Mwakilishi wake wa Kudumu
katika Umoja wa Mataifa, Balozi
Tuvako Manongi ni kiongozi wa
majadiliano ( lead negotiator) kuhusu
SDGs kwa Kundi la Afrika.
Pamoja na majadiliano ya jumla kuhusu mfumo wa tathmini na
ufuatiliaji, palikuwapo na mijadala ya pembezoni ( side events) iliyoandaliwa na wadau mbalimbali, moja ya mijadala hiyo ya pembezoni ni ule uliojadili nafasi za Ki Kanda
na Kitaifa katika mfumo wa ufuatiliaji na udhibiti, fursa na
changamoto za Malengo ya Maendeleo
Endelevu baada ya 2015 kwa upande wa Afrika.
Mjadala huo na ambao uliwashirikisha wadau mbalimbali
kutoka nchi wanachama na Asasi zisizo za Kiserikali uliandaliwa kwa ushirikiano kati ya Uwakilishi wa Kudumu wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa, Asasi za
Africa CSOs Working Group on Post 2015, Beyond 2015, Africa Development
Interchange Network na Africa Monitor.
Akichangia uzoefu wa Tanzania
katika eneo la tathmini na
Ufuatiliani, Afisa Mkuu wa Uwakilishi wa Kudumu, Bw.
Songelael Shilla, amewaeleza
washiriki wa mjadala huo kwamba, baadhi
ya mambo ambayo yalichangia kwa kiasi
Fulani udhaifu katika utekelezaji wa
Malengo ya Maendeleo ya Millenia
ni pamoja na ushirikishwaji hafifu wa jamii kuanzia ngazi ya wilaya, kata na .
Vile Matatizo
katika eneo la Takwimu eneo ambalo pia lilisababia migongano miongoni
wa makundi mbalimbali ya watendaji. Eneo jingine ambalo alilitaja kuwa limechangia
utekelezaji hafifu katika baadhi ya MDGs
ni ile la kutilia makazo
raslimali fedha kama ndio msingi mkuu wa
mafanikio ya MDGs.
Kwa sababu hiyo Afisa
huyo ambaye alizungumza kwa Niaba ya
Mwakilishi wa Kudumu wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa, alisema Tanzania inaamini na baada ya kujifunza na uzoefu uliotokana na utekelezaji wa MDGs, kwamba
mipango madhubuti, jumuishi na iliyowazi
katika mfumo wa ufuatiliaji na
tathimini ya utekelezaji
malengo ya maendeleo endelevu
baada ya 2015 utawezesha
utekelezaji wenye tija wa SDGs.
Baadhi ya wazungumzaji
katika mjadala huo walisisitiza pia
kwamba kama kweli Afrika inataka kupata mafanikio katika
utekelezaji wa SDGs basi haina budi
kuwekeza kwa wananchi wake ambao ndio wadau
na walengwa wakubwa wa SDGs hizo, wakasitiza pia umiliki wa mfumo huo na uwajibikaji wa wadau
mbalimbali kuanzia serikali , jumuiya ya kimataifa, asasi zisizo za kiserikali na wananchi kwa ujumla.
No comments:
Post a Comment