STATE HOUSE ZANZIBAR
OFFICE OF THE PRESS SECRETARY
PRESS RELEASE
Zanzibar 27.6.2015

RAIS wa
Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk. Ali Mohamed Shein jana
alishiriki futari ya pamoja na Wafanyakazi wa Wizara ya Nchi, Ofisi ya Rais
Ikulu na Utawala Bora, Wizara ya Nchi, Ofisi ya Rais Kazi na Utumishi wa Umma
pamoja na Wizara ya Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Idara Maalum za
SMZ.
Futari hiyo ya
pamoja ilifanyika katika viwanja vya Ikulu mjini Zanzibar ambapo pia,
ilihudhuriwa na viongozi mbali mbali akiwemo Makamo wa Kwanza wa Rais Maalim
Seif Sharif Hamad, Makamo wa Pili wa Rais Balozi Seif Idd, Spika wa Baraza la
Wawakilishi Mhe. Pandu Ameir Kificho, Kadhi Mkuu wa Zanzibar Sheikh Khamis
Haji, Katibu Mkuu Kiongozi na Katibu wa BLW Dk. Abdulhamid Yahaya Mzee na
viongozi wengine wa Serikali.
Akitoa neno la
shukurani kwa niaba ya Mhe. Rais mara baada ya futari hiyo, Waziri wa Nchi
Ofisi ya Rais Ikulu na Utawala Bora Mhe. Dk. Mwinyihaji Makame alisema kuwa
lengo la futari hiyo ni kupongezana kwa wafanyakazi na viongozi wa Wizara hizo
baada ya kupitishwa Bajeti za Wizara hizo katika Baraza la Nane la Wawakilishi lililofikia
kikomo chake hapo jana ambalo lilivunjwa rasmin na Rais Dk. Shein.
Dk. Mwinyi alitoa
pongezi hizo kwa niaba ya Rais kwa wafanyakazi na viongozi wa Wizara hizo kwa
kazi kubwa waliyoifanya katika kuhakikisha Wizara zao zinatekeleza majukumu
yaliokusudiwa kwa lengo la kupata maendeleo na mafanikio makubwa zaidi katika
Wizara hizo na Serikali nzima kwa juma.
Pia Dk. Mwinyi,
alitumia fursa hiyo kuwashukuru viongozi,wafanyakazi hao pamoja na waalikwa
wote kwa kuhudhuria futari hiyo maalum ya pamoja.
Rajab
Mkasaba, Ikulu Zanzibar
Postal Address: 2422 Tel.:0777427449. Fax: 024
2231822
E-mail:
rajabmkasaba@yahoo.co.uk
No comments:
Post a Comment