Na Maryam Kidiko Maelezo-Zanzibar
.
Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar pamoja na jeshi la Polisi watafanya Doria za mara kwa mara ambazo zitakuwa endelevu pamoja na kuwakamata Wahalifu wote wanaofanya vitendo vya kutumia Mihadarati pamoja na Pombe za kienyeji jambo ambalo hupelekea kuathiri afya zao na Vijana kujiingiza katika ngono zembe ambayo husababisha maambukizi mpya kwa Vijana hao.
Akijibu suali la Muwakilishi wa Jimbo la Wawi Saleh Nassor Juma huko Baraza la Wawakilishi Chukwani Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamo wa Kwanza wa Raisi Fatma Abdulhabib Fereji amesema Tume ya Ukimwi kupitia mpango shirikishi wa Jamii kwa kupambana na Ukimwi ilianzisha Kamati maalum na kujenga uwezo ili iweze kufanya kazi ya kutoa Elimu, Ushauri nasaha na pia kupeleka huduma za upimaji wa VVU Kwa Jamii katika Maeneo hayo.
Amesema kuwa Tume ilihamasisha kuanzisha Kikundi cha Polisi Jamii ili kujenga uwezo kwa kupitia mafunzo ya kufikisha Elimu ya Ukimwi pamoja na athari za Dawa za kulevya.
Vilevile amefafanua kuwa kutokana na Changamoto zilizopo, Tume inakusudia kuanzisha Kamati ya Ulinzi na usalama ya Mkoa wa Kusini Pemba ili iweze kutambua tatizo liliopo katika Kijiji hicho.
Wakati huo huo Naibu Waziri wa Habari Utalii Utamaduni na Michezo Bihindi Hamad Khamis amesema kipindi cha zaidi ya Miaka (40) Rais wa Ujerumani ni Kiongozi wa Kwanza kutumia utaratibu wa Boti au Meli na baadae kutembea kwa Miguu kutoka Bandarini.
Hayo ameyasema huko katika Ukumbi wa Baraza la Wawakilishi ulioko Chukwani Nje kidogo na Mji wa Zanzibar wakati akimjibu Suala lake Muwakilishi wa Jimbo la Muyuni Jaku Hashim Ayoub aliyetaka kujuwa ni Viongozi wangapi wa Kimataifa walowahi kuingia na kutoka Zanzibar kwa kutimia utaratibu aliyotumia Raisi wa Ujerumani.
Aidha amesema kuwa Viongozi wa Kitaifa wanaposafiri na wanapotaka wenyewe hutumia Usafiri wa Boti kutoka Sehemu moja kwenda Sehemu nyengine.
“Siwezi kushauri Viongozi watumie usafiri wa Boti kwani kanuni na Miongozo ya Safari za Watumishi wote wa Umma wakiwemo Viongozi wa Kitaifa zinatolewa na Tume ya Utumishi Serikalini kwani huzingatia vigezo maalum vya Utumishi “ Alisema Naibu huyo.
Vile vile amesema Kiongozi yoyote akiondoka nchi moja kwenda Nchi nyengine kupitia usafiri wa Ndege hufika haraka pahali husika na kuweza kuwahi kutekeleza majukumu yaliyompeleka huko.
Hata hivyo amesema kutokana na Raisi huyo kufuatana na Vyombo vya Habari Vikubwa Duniani tutarajie Nchi yetu kuendelea kutangazwa zaidi Duniani pamoja na kuengezeka kiwango cha Watalii watakao kuja kutoka Ujerumani kwa kupitia Njia ya Baharini pamoja na Viwanja vya Ndege.
No comments:
Post a Comment