Wanawake wa Vikundi vya Ushirika Jimbo la Kitope wakimshangiria Mke wa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapindizi Mama Mwanamwema Shein, na Ujumbe wake wa Wake wa Wawakilishi na Wabunge wa CCM walipowasili katika viwanja vya mpira Kiwengwa Kombaurembo Mkoa wa Kaskazini Unguja.
Mke wa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mama Mwanamwema Shein, akisalimiana na Wananchi wa Kijiji cha Kiwengwa wakati akiwasili katika viwanja vya mpira Kiwengwa Kombaurembo kwa ajili ya kukabidhi misaada Vikundi vya Wanawake 32 vya Jimbo la Kitope Zanzibar.
Mwanafunzi Simai Mcha akisoma Quran wakati wa ufunguzi wa hafla hiyo ya Mke wa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mama Mwanamwema Shein, alipofika kutowa misaada kwa Wanawake wa Vikundi 32 vya Ushirika vya Kiwengwa Zanzibar.
Mwanakikundi Bi Asha Abdalla akisoma risala kwa niaba ya Vikundi 32 vya Ushirika vya Wanawake Kiwengwa wakati wa hafla ya kukabidhiwa misaada iliotolewa na Mke wa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi na Umoja wa Wawanawake wa Wake wa Viongozi wa CCM Wabunge na Wawakilishi wa CCM Zanzibar.
Mke wa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mama Mwanamwema
Shein, akiwahutubia Wanawake wa Vikundi vya Ushirika 32 vilioko Kiwengwa wakati
wa kukabidhi misaada kwa vikundi hivyo. Hafla hiyo imefanyika katika viwanja
vya mpira kombaurembo kiwengwa.
Wananchi wakishangiria wakati wa hutuba ya Mama Mwanamwema Shein, akihutubia
Wananchi wa Kiwengwa wakimsikiliza Mke wa Rais wa Zanzibar akiwahutubia wakati wa hafla ya kukabidhi msaada wa fedha kwa Wajasiriamali wa Vikundi vya Ushirika vya Wanawake Kiwengwa Zanzibar
Wazee wa Kijiji cha Kiwengwa Mkoa wa Kaskazini Unguja wakimsikiliza Mke wa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi akiwahutubia katika viwanja vya mpira kombaurembo kiwengwa.
Mke wa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mama Mwanamwema
Shein, akimkabidhi msaada wa fedha Kiongozi wa kikundi cha Tuwe Macho Ngombeni
kiwangwa Bi Siwageni Nyange, akipokea kwa niaba ya kikundi chake hafla hiyo
imefanyika katika viwanja vya mpira kombaurembo kiwengwa.
Mke wa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mama Mwanamwema Shein, akimkabidha fedha Kiongozi wa Kikundi cha Tusife Moyo Bi Khadija Hamad, kwa ajili ya kutunisha mtaji wa kikundi chao, jumla ya vikundi 32 vya Ushirika vya Wanawake Wajasiriamali wamefaidika ma msaada huo
Wananchi wa kijiji cha Kiwengwa wakishangilia wakati wa hafla hiyo ya kukabidhiwa fedha na Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mwanamwema Shein, katika viwanja vya Kombaurembo Kiwengwa.
Mke wa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mama Mwanamwema Shein, akimkabidhi fedha Kiongozi wa Kikundi cha Tupendane Upenja, Bi Jina Haji kwa ajili ya kutunisha mtaji wa kikundi chao
Wananchi wa Kikjiji cha Kiwengwa Komba urembo wakimzawadia zawadi Mama Mwanamwema Shein, baada ya mkutano wake na Wanawake wa Vikundi vya Ushiriki vya Wanawake wa Kiwengwa Zanzibar.
Maalim akisoma dua baada ya kumalizika kwa hafla ya kukabidhi misaada kwa Wajasiriamali Wanawake wa Vikundi vya Ushirika Kiwengwa Zanzibar, hafla hiyo imefanyika katika viwanja vya mpira Kombaurembo Kiwengwa.
No comments:
Post a Comment