Habari za Punde

Wavuvi kutoka Comoro waliopotea tokea Mei 11 waonekana Bahari ya Mkoani

WATU wanaodhaniwa kuwa ni wavuvi ambao ni raia wa visiwa vya Comoro, waki nje ya hospitali ya Abdalla Mzee Mkoani Pemba, wakiwa na furaha baada ya kupatiwa matibabu, kufuatia kubururuwa na maji tokea Mei 11, mwaka huu na kuonekana juzi Juni 24 bahari ya Mkoani Pemba, (Picha na Haji Nassor, Pemba).
 SAMAKI waliokuwa wamekaushwa kwa jua ambao walikuwa wanakula wavuvi sita wa Comoro, ambao walipotea kwa kubururwa na maji tokea Mei 11, mwaka huu hadi kuoneakana juzi,  Juni 24 mwaka huu bahari ya Mkoani Pemba, (Picha na Haji Nassor, Pemba)
 WATU wanaodhaniwa kuwa ni wavuvi ambao ni raia wa visiwa vya Comoro, wakiwa ndani ya boti yao aina ‘Fiber’ wakifanya usafi, baada ya kuokotwa juzi bahari ya Mkoani, tokea walipopotea kutoka kwao, Mei 11  mwaka huu, ambapo hali zao ni nzuri, wakisubiri taratibu za nchi na kurudi kwao, (Picha na Haji Nassor, Pemba).
 BAADHI ya wananchi na watendaji wa uhamiaji wilaya ya Mkoani, wakiangalia boti iliokuwa imewabeba wavuvu raia wa Comro, wakiwa bandari ya Mkoani Pemba, wakifanya usafi, ambapo wavuvi hao walipotea tokea Mei 11 mwaka huu na kuoneana Juni 24 katika bahari ya Mkoani, (Picha na Haji Nassor, Pemba)
MSAIDIZI nahodha wa ‘fiber’ iliokuwa imebeba wavuvi sita wa Comoro na kupotea tokea Mei 11 na kuoneakana juzi bahari ya Mkoani Pemba Yunnus Maishe Mussa, ambae anazungumza Kiswahili taratibu, akizungumza na waandishi wa habari juu ya mkasa uliowakumba, (Picha na Haji Nassor, Pemba)


No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.