Afisa Mipango , Utekelezaji na Ufuatiliaji wa Mfuko wa
Hifadhi ya Jamii Zanzibar (ZSSF) , Khalifa Muumin Hilal,akielezea jinsi mfuko wa ZSSF unavyotowa huduma za Mafao kwa Wanachama wake
Maofisa Utumishi na Mipango wa Ofisi za Serikali na Binafsi wakimsikiliza Ofisa wa ZSSF wakati wa mkutano wa kutowa Elimu ya Mafao ya Uzazi kwa Wanachama wake.
Afisa Mipango , Utekelezaji na Ufuatiliaji wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii Zanzibar (ZSSF) , Khalifa Muumin Hilali, amewahakikishia Wananchi na Watoto kwa ujumla kuwa Watafaidika na matumizi ya Kiwanja cha Kufurahishia Watoto kilichoko Tibirinzi Kisiwani Pemba, katika Sikukuu ya IdilFitri inayokuja kwa vile Ujenzi wake umeshafikia asilimia 98%.
Afisa Mipango , Utekelezaji na Ufuatiliaji wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii Zanzibar (ZSSF) , Khalifa Muumin Hilali, amewahakikishia Wananchi na Watoto kwa ujumla kuwa Watafaidika na matumizi ya Kiwanja cha Kufurahishia Watoto kilichoko Tibirinzi Kisiwani Pemba, katika Sikukuu ya IdilFitri inayokuja kwa vile Ujenzi wake umeshafikia asilimia 98%.
Akizungumza na mwandishi wa Habari hizi huko Kiwanjani
Tibirinzi nje kidogo ya Mji wa Chake Chake Kisiwani humo, alisema ujenzi huo
unatarajiwa kukamilika muda mfupi ujao kwa vile Pembea zote Tano zimeshafungwa
na Umeme mkubwa ambao ulikuwa ni kikwazo cha kuzifanyia majaribio
Mashine
zilizopo Kiwanjani hapo tayari mafundi wako hatuwa za mwisho kumaliza kuunga.
Hilali, alieleza kuwa kazi kubwa iliobakia kwa sasa ni
usafishaji wa kiwanja ambao unaendelea na umaliziaji wa Ujenzi wa Barabara ya
Ndani ya Kiwanja ambayo imefikia hatuwa ya umaliziaji ambapo Mafundi
walihakikisha kuwa kabla ya kumi la kwanza kumalizika watakuwa wameshamaliza
kazi hiyo na tayari kwa matumizi.
“Tatizo letu kubwa tulilokuwa nalo ni Umeme wa Uhakika ( mkubwa
) na tayari mafundi wapo na wameshafunga Transfoma na mashine nyengine na Waya
umeshafika Kiwanjani kutokea Wesha ni kiasi cha kuunganisha tu kwa majaribio na
Pembea iliobakia mafundi wa Kichina wanasubiri kukamilika kwa uunganishaji wa
Umeme wamalize kufunga na kufanya majaribio,” alisema .
Kwa Upande wa Meneja wa Mfuko huo Pemba, Rashid Abdalla
Moh’d, alisema kuwa kazi iliobakia ni ndogo nan i ukweli Kiwanja hicho kitatumika
kwa Sikukuu ya IdilFitri inayokuja , baada ya watoto kukikosa kwa muda mkubwa
sasa kwa vile ujenzi umefikia hatuwa za mwisho.
Akizungumzia suala la bei ya Kiwanja kwa mtu atakae ingia ,
alieleza kuwa ni Tshs 1,000/= kwa Mtu mzima na 500/= kwa mtoto na hiyo haina
utafauti baina ya Unguja na Pemba.
“ Tatizo letu lilikuwa ni Umeme mkubwa kwa vile hivi Vifaa
haviwezi kwenda kwa Umeme mdogo uliokuwepo na tayari mafundi kutoka Kampuni ya
Molel Electrical Contractors Ltd ya Dar-es-Salaam wanamalizia kuunganisha
kutoka Waya unaotoka Wesha hadi humu ndani,” alieleza.
Nae Fundi Umeme kutoka Kampuni hiyo kutoka Kampuni hiyo,
Engineer , Rwegoshora Clavers, aleleza kuwa kazi ya kuingiza Umeme ndani ya
Kiwanja tayari imefikia hatuwa mzuri na tayari wameshafunga Transfomer kubwa
Kiwanjani hapo na tayari wamesha unganisha na Mashine nyengine za kuendeshea
Mashine za Kiwanjani hapo.
“ Wananchi wasiwe na Wasi wasi Shughuli ya Umeme imekamilika
na tunawaahidi Kiwanja watakitumia bila ya Wasiwasi wowote,” alieleza Engineer
huyo.
Watoto wa Kisiwa cha Pemba , wamekosa kufurahia Sikukuu
katika Kiwanja hicho kwa muda mkubwa tokea pale Mfuko wa Hifadhi ya Jamii ZSSF
, kuamuwa kukifanyia matengenezo makubwa.
No comments:
Post a Comment