Wasanii wa Kikundi cha Tausi Kilicho chini ya Gwiji la Sanaa Nchini Bibi Maryam Hamdan kikitoa burdani ya Maulidi ya Homu kwenye uzinduzi wa Tamasha la 18 la Filam la Nchi za Jahazi Zanzibar { ZIFF } hapo Hoteli ya Double Tree By Hilton Shangani Mjini Zanzibar.
Mkurugenzi wa Tamasha la Filam la Nchi za Jahazi Zanzibar { ZIFF } Profesa Martin Mhando akitoa neneo la makaribisho kwenye uzinduzi wa Tamasha hilo hapo shangani.
Meneja wa Taasisi ya Kimataifa inayosimamia kukuza vipaji vya wasanii katika ukanda wa Afrika Mashariki { ZUKU } Bibi Maud Roger akiahidi taasisi yake kuendelea kusaidia vipaji vya vijana katika utengenezaji wa filam zilizo bora Nchini.
Baadhi ya washirika wa Tamasha la Filam la Nchi za Jahazi Zanzibar { ZIFF } waliohudhuria uzindazi wake kutimia miaka 18 tokea kuasisiwa kwa Tamasha hilo hapa Nchini.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif wa Pili kutoka Kushoto akiwa mgeni rasmi kwa Niaba ya Rais wa Zanzibar Dr Ali Mohammed Shein akijumuika pamoja na baadhi ya viongozi kwenye uzinduzi wa Tamasha la 18 la Filam la Nchi za Jahazi Zanzibar hapo Double Tree By Hilton Shangani Mjini Zanzibar.
Kulia ya Balozi Seif ni Waziri wa Habari, Utamduni, Utalii na Michezo Mh. Said Ali Mbarouk, kushoto ya Balozi Seif ni Mwenyekiti wa Bodi ya ZIFF Mh. Mhmoud Thabit Kombo na msanii wa filam ya sarafina kutoka Nchini Afrika Kusini Laleta Kumalo.
Mwenyekiti wa Bodi ya Tamasha la Filam la Nchi za Jahazi Zanzibar { ZIFF } Mahmoud Thabit Kombo akitoa neon la kumkaribisha mgeni rasmi kulizindua Tamasha hilo hapo Double Tree By Hilton Shangani.
Msanii Mkongwe wa nyimbo kutoka Johannesburg Nchini Afrika Kusini Doroth Masuka akipongeza juhudi zinazochukuliwa na Serikali pamoja na washirika wake katika kuimarisha vipaji vya wasanii hapa Nchini.
Balozi Seif akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya Viongozi na washirika wa Tamasha la Filam la Kimataifa la Nchi za Jahazi mara baada ya kulizindua Tamasha hilo kwa niaba ya Rais wa Zanzibar Dr. Ali Mohammed Shein.
Kulia ya Balozi Seif NI Waziri wa Habari, Utamaduni, Utalii na Michezo Mh, Said Ali Mbarouk na Meneja wa Taasisi ya Kimataifa inayosimamia kukuza vipaji vya wasanii katika ukanda wa Afrika Mashariki { ZUKU } Bibi Maud Roger.
Kushoto ya Balozi Seif ni Mwenyekiti wa Bodi ya Tamasha la Filam la Nchi za Jahazi Zanzibar { ZIFF } Mahmoud Thabit Kombo pamoja na Msanii Maarufu Duniani aliyeigiza filam Maarufu ya Mchezo wa sarafina kutoka Nchini Afrika Kusini Bibi Laleta Kumalo.
Picha na – OMPR – ZNZ.
No comments:
Post a Comment