Habari za Punde

Balozi Seif Akikata Utepe Kuashiria Kulifungua Jengo la Tume ya Taifa ya Sayansi

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akilifungua rasmi Jengo Jipya la Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia Tanzania { COSTECH } Ofisi ya Zanzibar liliopo ndani ya majengo ya zamani ya ilichokuwa kiwanda cha Sigara Maruhubi Nje kidogo ya Mji wa Zanzibar.
Balozi Seif wa pili kutoka Kushoto akipata maelezo kutoka kwa Wataalamu  wa Chuo cha Utafiti Kizimbani  wakiongozwa na Said Suleiman Bakari jinsi zao la viazi vitamu linavyoweza kutumiwa vyema katika utengenezaji wa Juisi.Wa kwanza kutoka kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Majini Magharibi Mh. Abullah Mwinyi.
Watafiti na wawakilishi wa Vikundi vya wajasiri amali waliopata ufadhili kutoka Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia wakimpatia maelezo Balozi Seif wakati akiangalia maonyesha mara baada ya kulifungua Jengo la Tume hiyo.
Balozi Seif akizungumza kwenye hafla ya uzinduzi wa Jengo la Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia hpo Maruhubi akimuwakilisha Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la MapinduziI Dr. Ali Mohammed Shein.


 Balozi Seif akiwa katika Picha ya pamoja na wajumbe wa Bodi ya Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia Tanzania { COSTECH } mara baada ya uzinduzi wa jengo la Tume hiyo hapo Maruhubi.
Kulia ya Balozi Seif ni Kaimu Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar M,h. Ali Juma Shamuhuna, Mkurugenzi Mkuu wa Costech Dr. Hassan Mshimba, Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Taifa Zanzibar {SUZA} Dr. Idriss Rai.
Kushoto ya Balozi Seif ni Mwenyekiti wa Bodi ya Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia Kanal MstaafuJoseph Simba Kalia, Mkuu wa Mkoa Mjini Magharibi Mh. Abdullah Mwinyi pamoja na Naibu Katibu Mkuu Osifi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Nd. Ahmad Kassim.
Picha na – OMPR – ZNZ.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.