Habari za Punde

Fidel Castro bingwa CCM ‘Cup’ Wawi

Na Haji Nassor, Pemba
TIMU ya Fidel castro, imefanikiwa kutazwa bingwa wa michuano ya kuwania kombe la jimbo la Wawi CCM, baada ya kuipokonya tonge mdomoni, bingwa mtetezi timu ya Wawi star kwenye fainali kali iliochezwa uwanja wa Gombani.
Katika ngarambe hiyo ilioshuhudiwa na waziri wa mawasiliano, sayansi na teknolojia wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Pro: Makame Mnyaa Mbarawa, timu ya Wawi star iliongoza goli moja tokea dakika 15, kwa goli lilifungwa na Azhar Mbarouk.
Dakika ya 80 ikiwa tayari Wawi star wameshajihakikisha kutetea ubingwa mwao, Ramadhan Said alisawazisha goli hilo, kwa mkwaju mkali, baada ya kutokezea adhabu ndogo, ambapo baadae sheria ya mikwaju ya penalti ilitawala.
Katika hilo, timu ya Fidel castro iliingiza penalti nne, huku wapinzania wao wakifanikiwa kupoteza mbili na kufunga mbili, ambapo baadae Fidel castro wakaibuka washindi kwa magoli 5-3.
Katika mashindano hayo, mshindi alikabidhiwa seti mbili za jezi, mipira miwili na kitita cha shilingi 300,0000, huku makamu bingwa akikabidhiwa seti mbili za jezi, mpira mmoja na shilingi 150,000 wakati mshindi wa tatu timu ya Furaha,ikikabidhiwa seti moja, mipira na shilingi 100,000.
Akizungumza kabla ya kugawa zawadi hizo Waziri huyo wa Mawasiliano Pro: Makame Mnyaa Mbarawa, alisema sasa michezo imekuwa sio burudani pekee, bali huzaa ajira endelevu.
Nae mlezi wa Michuano hiyo Daud Is-mail Juma alisema michuano ijayo anatarajiwa kuimarisha zaidi kwa kuweko Ng’ombe wa maziwa ili vilabu vijiongezee pato lao.

Michuano ya kombe la CCM Jimbo la Wawi, ambayo iliasisi mwaka 2009, na kuvihusisha vilabu pekee vinavyotambuliwa na ZFA, kwa msimu huu iliohusisha vilabu tisa vya Jimbo la Wawi, ambavyo baadhi havina usajii, akiwemo bingwa wa msimu huu.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.