Pichani ni
Katibu Mkuu, Balozi Liberata
Mulamula akiwa na Balozi Ramadhan
Mwinyi, Naibu Mwakilishi wa Kudumu wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa.
Katibu
Mkuu, Wizara ya Mambo ya Nje na
Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi
Liberata Mulamula, amewaaga watanzania waishio nchini Marekani,
kwa kuwataka kujivunia utanzania wao na kutoionea aibu lugha yao ya
taifa, Kiswahili.
Mwishoni
mwa wiki, Ubalozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Marekani, uliandaa hafla ya aina yake ya
kumpongeza, kumshukuru na kumuaga
Balozi Liberata Mulamula ambaye
sasa ni Katibu Mkuu, Wizara ya Mambo ya
Nje na Ushirikiano wa Kimataifa.
Hafla
hiyo iliyowajumuisha watanzania wa kada
mbalimbali wakiwamo maafisa na
wafanyakazi wa Uwakilishi wa Kudumu wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa, wakiongozwa na Balozi
Ramadhan Mwinyi, ilipambazwa kwa nasaha mbalimbali na salamu
za kumtakia kheri Balozi Mulamula katika
jukumu lake jipya.
Pamoja
na kusikiliza salamu kutoka kwa wawakilishi
wa makundi ya kijamii,
na kupokea zawadi, Katibu Mkuu, Balozi Mulamula naye alipata
fursa ya kuzungumza mawili matatu.
Katika salamu zake kwa watanzania
waliojumuika katika makazi yake.
Moja ya mambo muhimu
aliyoyazungumza ni pamoja na kuwaasa
watanzania waishio nchini
Marekani, kujivunia utanzania wao,
umoja wao na kubwa zaidi kutoona aibu kuizungumza na kuiendeleza lugha
ya taifa Kiswahili.
“Niwaombeni jambo moja,
msione aibu kuzungumza lugha yetu, lugha yenu ya Kiswahili, miaka kadhaa iliyopita watanzania waughaibuni walikuwa hawazungumzi Kiswahili , waliogopa kujitambulisha kwa
lugha yao, lakini sasa hali imebadirika
sana, unakutana na watanzania kila kona
wanazungumza Kiswahili hili ni jambo la
kujivunia sana na ninawaomba tuendeleze
utamaduni huu wa kuzungumza Kiswahili, kuwa ugenini hakumaainishi uachane na
lugha yako” akasisitiza Balozi Mulamula na kushangiliwa na watanzania.
Katika kutilia mkazo
wa lugha ya Kiswahili, Balozi
Mulamula aliwataka wana DMV kuendelea na darasa la kuwafundisha
watoto lugha hiyo ya Kiswahili na maeneo mengine kuiga mfano huo.
Jambo jingine ambalo Balozi alililowasisitizia watanzania hao ni kuhusu upendo, mshikamano,
kuheshimiana, kusaidia na kutobaguana kwa misingi ya dini, kabila, eneo
ambalo mtu anatoka au kwa misingi
ya itikadi za kisiasa.
“
Ninaondoka baada ya miaka miwili ya
kuwa Balozi wenu, na katika miaka hii miwili nimejifunza mengi
sana kutoka kwenu, mmeshirikiana nami na
Ubalozi katika mambo mengi yakiwamo ya kuchangia maendeleo yenu wenyewe na
maendeleo ya watanzania wenzenu endeleeni na moyo huu”.,
Kaongeza
“nitakuwa nanyi na kama mjuavyo tunakitengo kizima kinachoshughulia masuala ya
diaspora, na kama ningekuwa mwanasiasa basi
nyie wanadiaspora mngekuwa mtaji
wangu, jimbo langu”. akabainisha na
kuamsha tena vifijo kutoka kwa
wana-diaspora hao.
Katika
hatua nyingine, Katibu Mkuu, Balozi Mulamula amewahimiza watanzania walioko nje, kumchangamkia hasa kwa wale wenyekutaka kujaza fomu za
maombi ya pasi zao za kusafiria ambazo zimekwisha muda.
No comments:
Post a Comment