Habari za Punde

Kinyang'anyiro cha Uwakilishi Jimbo Jipya la Chukwani Zanzibar


Msimamizi wa Mkutano wa Uchaguzi akitowa maelekezo kwa Wananchi na Wagombea wakati wa mkutano huo wa kampeni uliofanyika Tawi la CCM Mitindooni 
Mgombea nafasi ya Uwakilishi Ndg Juma Rajab akijieleza kwa Wananchi wa Tawi la CCM Mitondooni wakati wa kuomba ridhaa za Wananchi wa Jimbo hilo jipya la Uchaguzi Zanzibar.
Wananchi wa Tawi la CCM Mitondooni wakifuatilia mkutano huo wa Kampeni kwa Wagombea wa Uwakilishi. 
Akiomba Kura Ndg Thabit Jecha Thabit Kombo kwa wananchi wa tawi la ccm mitondooni ili kupata ridhaa kuliwakilisha jimbo hilo jipya la uchaguzi Zanzibar.
Mgombea Nafasi ya Uwakilishi kupitia Jimbo Jipya la Chukwani Ndg Thabit Jecha Kombo akiomba kura kwa Wananchi wa Jimbo la Chukwani wakati wa mkutano wa kampeni katika tawi la ccm mitindooni wilaya ya magharibi unguja 
Wananchi wa Tawi la CCM Mitondooni wakiwasikiliza Wagombea wa Uwakilishi katika Jimbo hilo jipya la Uchaguzi wakati wa mkutano wa kampeni tawini hapo,
Mgombea Uwakilishi Jimbo Jipya la Chukwani Ndg Ramadhani Mrisho Rupia akijinadi kwa Wananchi wa Tawi la CCM Mitondooni wakati wa mkutano wa Kampeni katika tawi hilo kuiomba ridhaa za wananchi kuweza kumteuwa kugombea nafasi hiyo katika jimbo hilo jipya.
Mgombea nafasi ya Uwakilishi Ndg Mwanahamis Khamis Juma akijieleza wakati wa kuomba kura kwa Wananchi wa Tawi la CCM Mitondooni Wilaya ya Magharibi Unguja  
Kada wa CCM na Waziri Mstaafu wakati wa awamu ya Sita Ndg Asha Abdalla Juma akijinadi kwa Wananchi wa Tawi la CCM Mitondooni wakati wa kampeni ya kuwania jimbo hilo jipya la Chukwani. 
Mgombea Uwakilishi Jimbo Jipya la Chukwani Zanzibar Ndg Jamal Mohammed Mikidadi akijieleza kwa Wananchi wa Tawi la CCM Mitondooni wakati wa mkutanbo wa Kampini kuwania nafasi hiyi katika Jimbo hilo la Chukwani, Na kutoa ahadi endapo atapata ridhaa za wananchi atatowa papaumbele kwa Vijana kujiendeleza kwa Elimu ya Juu na kuimarisha Vikundi vya Wanawake vya Ushiriki kujipatia kipato na kuhakikisha jimbo hilo linakuwa juu kwa maendeleo

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.