Habari za Punde

Kojani waaswa kuunga mkono jitihada za kupamabana madawa ya kulevya,ukimwi na utunzaji wa mazingira

Na Haji Nassor, PEMBA

WANANCHI wa kijiji cha Kojani wilaya ya Wete, wametakiwa kuunga mkono juhudi zinazochukuliwa na Jumuiya ya Kojani inayopambana na madawa ya kulevya, maambukizi mapya ya virusi vya Ukimwi na utunzaji wa mazingira ‘KOYMOCC’ katika kuuweka mtaa huo safi.

Wito huo umetolewa na Mwenyekiti wa Jumuiya hiyo nd: Hamad Ali Mussa, katika uzinduzi wa usafi wa mazingira kijijini huko uliohusisha shehia za Mpambani na Kojani yenyewe mara baada ya kupatiwa mafunzo kupitia mradi wa elimu juu ya usafi wa mazingira.

Alisema kuwa, endapo wananchi hao wataunga mkono juhudi hizo wanaweza kufanikiwa na kufikia lengo kwa vile wao ndio walengwa wakuu wa mradi huo.

Alieleza kuwa usafi ni kitu muhimu katika maisha ya kila siku ya binadamu hivyo ni vyema kwa wananchi hao kushirikiana bega kwa bega katika kufanikisha zoezi hilo.

‘’Jamani usafi ni ktu pekee kwani kinamfanya mtu na hata jamii kuijumla ipendeze lakini pia hata dini yetu ya kiislamu imehimiza kitu usafi’’, alisema Mwenyekiti.


Nae Katibu wa Jumuiya hiyo nd: Bakar Suleiman Juma alisema kuwa mradi huo wa elimu juu ya usafi wa mazingira umekuja wakati muafaka kijijini huko na kuwataka wananchi hao kuufanyia kazi.

Alifafanua kuwa suala la usafi wa mazingira ni jukumu la kila mmoja hivyo ni vyema kwa jamii kuweza kulielewa hilo sambamba na kulifanyia kazi.

‘’Mradi huu umekuja kwaajili yenu wananchi wa kojani na juhudi hizi za kuufikisha mradi kwenu umefanywa na ‘’KOYMOCC’ hivyo munapaswa kuzithamini juhudi zetu’’, alieleza.

Mmoja kati ya wananchi hao, Kheri Mrakib Mbarouk alisema aliipongeza Jumuiya ya ‘KOYMOCC’ kutokana na juhudi kubwa waliyoifanya ya kuwapatia mradi huo kwa vile ni faraja kwao katika kukibadilisha kijiji chao.

Nae Mwakanda Said Mbwana, alisema kuwa watakuwa mstari wa mbele katika kufanikisha zoezi hilo sambamba na kuiyomba Jumuiya kuwapatia vifaa kwaajili ya usafi.


Mradi huo wa elimu juu yausafi wa mazingira umefika kijiji huko kupitia Jumuia ya Koymocc chini ya ufadhili wa Foundation for Civil Socierty na utachukuwa kipindi cha mwaka mmoja.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.