Habari za Punde

Maalim Seif achukua Fomu leo kugombea Urais wa Zanzibar kwa tiketi ya CUF

Mgombea Urais kwa tiketi ya CUF, Maalim Seif Sharif Hamad akiwa na mgombea wa Urais wa Tanzania Mh Edward Lowassa leo katika ukumbi wa Salama  Bwawani..Mh Lowassa alimsindikiza Maalim Seif Shariff Hamad kwenda kuchukua fomu.
 Viongozi na wageni maalum walimsindikizMgombea Urais kwa tiketi ya CUF, Maalim Seif Sharif Hamad kwenye hafla ya uchukuwaji fomu.Kutoka kushoto ni Bi Fatma Fereji, Mhe Abubakar Khamis Bakary, Mzee hassan Nassor moyo, Mgombea mweza wa Urais Tanzania, Mhe juma Duni na mgombea urais wa tanzania kupitia UKAWA mhe Edward Lowassa.
DSC01631
Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar MH. Jecha Salum Jecha kwa makini akionesha fomu ya uteuzi kwa wananchi kabla ya kumkabidhi mgombea wa Urais kwa tiketi ya Chama Cha Wananchi CUF MH Maalim. Seif Sharif Hamad. Leo tarehe 23/08/2015 Salama Hall Bwawani Zanzibar.DSC01635
Makamo wa Kwanza wa Rais ambae pia ni Mgombea wa Urais kupitia Chama Cha Wananchi CUF, MH Maalim. Seif Sharif Hamad akipokea fomu za Uteuzi kutoka kwa Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar MH: Jecha Salum Jecha tarehe 23/08/2015 katika ukumbi wa Hoteli ya Bwawani Malindi Mjini Zazibar
 Mgombea Urais kwa tiketi ya CUF, Maalim Seif Sharif Hamad akionesha fomu za kugombea Urais mara alipokabidhiwa na Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar
 Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar MH: Jecha Salum Jecha akitoa ufafanuzi kuhusu fomu za kugombea uchaguzi kabla ya kukabidhi kwa Mgombea wa CUF , Maalim Seif Shariff Hamad
Mgombea Urais kwa tiketi ya CUF, Maalim Seif Sharif Hamad akizungumza na wanahabri ( hawapo pichani) baada ya kuchukua fomu za kugomea Urais Zanzibar

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.