Habari za Punde

MATOKEO YA KURA ZA MAONI KWA MAJIMBO YA WILAYA YA AMANI UNGUJA.

Katibu wa CCM Wilaya Amani Ndg Abdalla Mwinyi akitowa matokeo ya Uchaguzi wa Kura Za Maoni kwa wagombea Uchaguzi kupitia CCM Majimbo Matano yalioko ndani ya Wilaya hiyo nayo ni Jimbo la Amani,Chumbuni,Mpendae,Kwamtipura na Magomeni.

Akitowa matokeo hayo mbele ya Wanachama wa CCM wa Wilaya hiyo katika viwanja vya Afisi hiyo huko Amani Unguja jana usiku na kuhudhuriwa na wagombea wa Majimbo hayo.

MATOKEO YA UBUNGE WA JIMBO LA AMANI

Matokeo ya Jimbo la Amani lilikuwa na Wagombea wawili nao ni Aliyekuwa Mbunge wa zamani wa Jimbo hilo Mhe Mussa Hassan Mussa na Hassan Rajab Khatib.

Mshindi wakwanza amepata kura hizo za maoni ni Mhe Mussa Hassan Mussa kwa kupata kura 1,622

Nafasi ya Pili imechukuliwa na Ndg Hassan Rajab Khatib amepata kura 374.

MATOKEO YA UWAKILISHI JIMBO LA AMANI

Kwa upande wa Uwakilishi katika Jimbo la Amani walikuwa Wanachama 4 waliogombea nafasi hiyo. 
Mshindi wa kinyanganyiro hicho cha kura ya maoni kwa nafasi ya Uwakilishi Mshindi wa kwanza Ndg Rashid Ali Juma kwa kupata kura 1145,

Nafasi ya Pili imechukuliwa na aliyekuwa mwakilishi wa jimbo hilo Ndg. Fatma Mbarouk Said kwa kupata kura 489. Kwa

Nafasi ya Tatu imechukuliwa na Ndg Ali Denge Makame na

Nafasi ya mwisho imeshikwa na mgombea Ndg Seif Amir Seif kwa kupata kura 70.

MATOKEO YA JIMBO LA CHUMBUNI UBUNGE.

Kwanafasi ya Ubunge Wanachama wa CCM waliojitokeza ni 4 , akiwemu Mbunge wa Jimbo hilo Mhe Perera Ame Silima, ameagusha katika nafasi hiyi na Kamanda wa Jimbo la Chumbuni Ndg Ussi Salum Pondeza (HAMJAD).

Mshindi wa kwanza katika kinyanganyiro hicho ameibuka Ndg Ussi Salum Pondeza HAMJAD kwa kupata kura 1,941

Mshindi wa Pili aliyekuwa Mbunge wa Jimbo hilo Mhe.Pepera Ame Silima aliyepata kura 1,278. Na

Nafasi ya Tatu katika Uchaguzi huo wa kura ya maoni imechukuliwa na Ndg Shaban Salum Jabir kwa kupata kura 790,
Mgombea wa aliyechukua

Nafasi ya Nne Ndg Hamid Mzee Haji. Kwa kupata kura 54.

MATOKEO YA UWAKILISHI JIMBO LA CHUMBUNI  

Kwa nafasi ya Uwakilishi Wanachama waliojitokeza kwania nafasi hiyo walikuwa 4

Mshindi wa kura za maoni katika jimbo hilo Ndg Miraj Khamis Mussa kwa kupata kura 1,758,

Nafasi ya Pili imechukuliwa na Ndu Sharif Ali Sharif kwa kupata kura 1,723,

Nafasi ya Tatu imeshikwa na Ndg Khamis Omar Seif kwa kupata kura 301 na

Nafasi ya mwisho imechukuliwa na Ndg Hafidh Haji Faki kwa kupata kura 232.

MATOKEO YA UBUNGE JIMBO LA MPENDAE.


Kwa nafasi ya Ubunge katika Jimbo la Mpendae wamejitokeza WanaCCM 3, kuwania nafasi hiyo

Mshindi wa Jimbo hilo ni Mbunge wa Zamani aliyekuwa akitetea nafasi yake Mhe Salim Hassan Turky kwa kupa ushindi wa kishindo kwa kupata kura 1,218,

Mshindi wa Pili katika kura za maoni Ndg Issa Kassim Issa

Nafasi ya Tatu na ya mwishom imechukuliwa na Ndg Andrea Saimon Mbinga, kwa kupata kura 29.


MATOKEO YA KURA YA UWAKILISHI JIMBO LA MPENDAE.

Aliyekuwa mwakilishi wa Jimbo hiloMhe Mohammed Said Mohammed Dimwa ameweza kutetea vyema kiti chake kwa kuibuka na ushindi wa kura 1,028,

Nafasi ya Pili imechuliwa na Ndg Omar Said Ameir kwa kupata kura 168, na

Nafasi ya Tatu imeshikiliwa na Bi Asha Said Shamte kwa kupata kura 116 na

Nafasi ya mwisho imechukuliwa na Ndg Ahmed Khamis Rajab kwa kupata kura 59.


MATOKEO YA UCHAGUZI WA UBUNGE JIMBO LA KWAMTIPURA.
Jimbo la Kwamtipura lilikuwa na wagombea 7 waliowania nafasi hiyo.

Mshindi wa kwanza wa nafasi hiyo ya Ubunge Ndg Mattar Ali Salum kwa kupata kura 938

Mshindi wa Pili wa nafasi ya Ubunge Ndg Ali Juma Mohammed (RAZA) kwa kupata kura 757.

Nafasi ya Tatu imeshikwa na Ndg Kheir Ali Khamis kwa kupata kura 404.

Nafasi ya Nne imechukuliwa na Ndg Faina Idarous Faina kwa kupata kura 164.
Nafasi ya Tano imeshikwa na Ndg Ali Machano Mussa kwa kupata kura 132.

Nafasi ya Sita imeshikwa na Ndg Ali Omar Said kwa kupata kura 70.

Na nafasi ya mwisho imeshikwa na Ndg Wanimo Bakari Wanimo kwa kupta kura 13. 

MATOKEO YA UWAKILISHI JIMBO LA KWAMTIPURA

Wagombea walikuwa 4 katika nafasi hiyo ya Uwakilishi

Mshindi wa kwanza katika Jimbo hilo amechaguliwa aliyekuwa mwakilishi wa Zamani Ndg Hamza Hassan Juma kwa ushindi wa kura 1,176.

Mshindi wa Pili amechaguliwa Ndg Khamis Abdalla Amour kwa ushindi wa kura 795.

Nafasi ya Tatu imeshikiliwa na Bi Salama Shaib Mohammed. Kwa kupata kura 432.

Nafasi ya Nne imechukuliwa na Ndg. Kassim Juma Omar kwa kupata kura 395.  


MATOKEO YA KURA ZA MAONI JIMBO LA MAGOMENI UNGUJA.
Kwa nafasi ya Ubunge waliojitokeza kuwania nafasi hiyo walikuwa 5

Mshindi wa kwanza katika kura hizo za maoni katika jimbo hilo ni Ndg Jamal Kassim Ali kwa ushindi wa kura 1,414.

Aliyechukuwa nafasi ya Pili katika uchaguzi huo Bi. Mwanahamis Kassim Said kwa kupata kura 746.

Nafasi ya Tatu imechukuliwa na Ndg Haji Ameir Haji (BossMpakia) kwa kupata kura 331.

Nafasi ya Nne imeshikwa na Ndg Mohammed Khamis Chombo aliyekuwa mbunge wa Jimbo hilo ameshindwa kutetea kiti chake kwa kupata kura 149. Katika uchaguzi huo wa kura ya maoni.

Na nafasi ya mwisho imechukuliwa na Bi Rahma Rashid Ahmed kwa kupata kura 52.


KWA NAFASI ZA UWAKILISHI KATIKA JIMBO LA MAGOMENI.


Mshindi katika nafasi ya Uwakilishi katika jimbo hilo la Magomeni Ndg Rashid Makame Shamsi kwa kupata kura 1,120.

Nafasi ya Pili imechukuliwa na Ndg Abdul-razak Suleiman kwa kupata kura 829.

Nafasi ya Tatu imeshikwa na Ndg Mahfoudh Abdalla Mohammed kwa kupata kura 645.

Nafasi ya Nne imeshikwa na Ndg Mzee Shirazi Hassan kwa kupata kura 279.

Nafasi ya Tano imeshikiliwa na Bi Hafsa Said Khamis kwa kupata kura 142.

Nafasi ya Sita imechukuliwa na Ndg Ali Jussa Alaiya kwa kupata kura 89.
  


No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.