MZEE mmoja ambae hakupatikana jina lake,
kutoka shehia ya Mchanga mdogo wilaya ya Wete Pemba, akiuliza suali juu ya
umiliki wa ardhi, kwa watendaji wa Kituo cha Huduma za Sheria Zanzibar ZLSC
tawi la Pemba, wakati walipofika shehiani hapo, kutoa msaada wa kisheri bila ya
malipo, wakiambatana na wanasheria wengine, (Picha na Haji Nassor, Pemba)
MWANASHERIA kutoka Afisi ya
Mkurugenzi wa Mashitaka ‘DPP’ kisiwani Pemba, Seif Mohamed Khamis akijibu
masualia mbali mbali hasa ya usalama barabarani, yalioulizwa kwa wananchi wa
shehia ya Mchanga mdogo wilaya ya Wete, wakati watendaji wa Kituo cha Huduma za
Sheria Zanzibar ZLSC, tawi la Pemba, walipofika kijijini hapo kutoa msaada wa
kisheria bila ya malipo, (picha na Haji
Nassor, Pemba).
AFISA Mipango wa Kituo cha Huduma za
sheria Zanzibar ZLSC tawi la Pemba, mwalimu Mohamed Hassan Ali, akifafanua
jambo kwenye mkutano wa wazi ulioandaliwa na ‘ZLSC’ wa kutoa msaada wa
kisheria kwa wananchi wa shehia ya Mchanga mdogo wilaya ya Wete Pemba bila ya
malipo, (Picha na Haji Nassor, Pemba).
WANANCHI wa Mchanga mdogo wilaya ya Wete
Pemba, wakisoma majarida maalumu yanayochapishwa na Kituo cha Huduma za Sheria
Zanzibar ZLSC, majarida hayo yaligawiwa wakati watendaji wa ZLSC, walipofika
shehiani hapo, kutoa msaada wa kisheria bila ya malipo ikiwa ni ziara yao kwa
wilaya nne za Pemba, (Picha na Haji Nassor,
Pemba).
No comments:
Post a Comment