Rais Jakaya Mrisho kikwete akiwa na Waziri wa Sheria na Katiba Dkt Asha-Rose Migiro, Jaji Mkuu Mhe Mohamed Chande Othman, Jaji Kiongozi Mhe Shaaban Ally Lilla na Katibu Mkuu kiongozi katika picha ya pamoja na Majaji wa Mahakama Kuu 13 na Jaji wa Mahakama ya Rufaa mmoja aliowaapisha Ikulu jijini Dar es salaam leo Agosti 5, 2015
PICHA NA IKULU
THE UNITED REPUBLIC OF TANZANIA
DIRECTORATE
OF PRESIDENTIAL COMMUNICATIONS
Telephone: 255-22-2114512,
2116898
Fax: 255-22-2113425
|
![]() |
PRESIDENT’S OFFICE,
STATE
HOUSE,
1 BARACK OBAMA ROAD,
11400
DAR ES SALAAM.
Tanzania.
|
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete leo,
Jumatano, Agosti 5, 2015, amewaapisha Majaji 14 akiwamo Jaji mmoja wa Mahakama
ya Rufani Tanzania katika sherehe iliyofanyika Ikulu, Dar es Salaam.
Rais
Kikwete aliwateua majaji hao hivi karibuni katika mwendelezo wake wa
kuhakikisha kuwa Muhimili wa Mahakama unakuwa na raslimali watu ya kutosha ili
kuendelea kutoa haki kwa haraka zaidi na kwa ufanisi zaidi.
Walioapishwa
leo katika sherehe iliyohudhuriwa pia na Jaji Mkuu wa Tanzania, Mheshimiwa
Mohamed Chande Othman ni pamoja na Jaji Richard Mziray ambaye anakuwa Jaji wa
Mahakama ya Rufani ya Tanzania.
Majaji
wengine ambao wote ni Majaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania ni Mheshimiwa Ignas
Pius Kitusi, Mheshimiwa Lameck Michael Mlacha, Mheshimiwa Wilfred Peter
Dyansobera, Mheshimiwa Salima Mussa
Chikoyo, Mheshimiwa Issa Kweka Arufani, Mheshimiwa Sirilius Betran Matupa na
Mheshimiwa Julius Benedicto Malaba.
Wengine ni
Mheshimiwa Victoria Lyimo Makani, Mheshimiwa Lucia Gamuya Kairo, Mheshimiwa
Rehema Joseph Kirefu, Mheshimiwa Benhaji Shaaban Masoud, Mheshimiwa Issa John
Maige na Mheshimiwa Adam Juma Mwambi.
Imetolewa
na:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya
Rais,
Ikulu,
DAR
ES SALAAM.
5 Agosti, 2015
No comments:
Post a Comment