Habari za Punde

Rais wa Zanzibar Dk Shein Azinduzi wa Barabara ya Wete Gando Pemba.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein, akikata utepe kuzindua barabara ya Wete Gando na Wete Konde,kushoto Naibu Waziri wa Wizara ya Miundombinu na Mawasiliano Zanzibar Issa Haji Gavu. 
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein, akiondoa kipazia kuashiria kuzindua barabara za Wete Gando na Wete Konde, akiwa katika ziara yake Kisiwani Pemba.kuzindua miradi ya maendeleo kisiwani humo.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi akiwapungia mkono wananchi wa Wete wakati akitembelea barabara hiyo baada ya kuifungua baada ya kumalizika ujenzi wake uliofanywa na Kampuni ya Ujenzi ya MECCO Tanzania.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Shein, akikagua barabara hiyo baada ya kuifungua rasmin na kutowa huduma ya usafiri kwa wananchi wa Wilaya ya Wete Pemba.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi akiwasalimia Wananchi wa Wilaya ya Wete wakati wa kutembelea barabara hiyo baada ya kuifungua.kulia Katibu Mkuu Wizara ya Miundombinu na Mawasiliano Zanzibar Dk Juma Akili na kushoto Naibu Waziri wa Wizara ya Miundombinu na Mawasiliano Mhe Issa Haji Gavu.
Katibu Mkuu Wizara ya Miundombinu na Mawasiliano Zanzibar Mhe Juma Akali akitowa maelezo ya Ujenzi wa barabara za Wete Gando wakati wa ufunguzi huo uliofanywa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein, 
Mwakilishi wa Mfuko wa Saudia Fund Ibrahim Al-Sugair, akitowa salamu za Serikali ya Saudia wakati wa ufunguzi wa barabara hiyo iliojengwa kwa Msaada wa Mfoko huo na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, uzinduzi huo umefanyika katika viwanja vya kijiji cha Gando Wete Pemba. 

Mwenyekiti wa Bodi ya Kampuni ya MECCO Tanzania Ndg Obadiah Kwabhi akitowa shukrani kwa ushirikiano wa kufanikisha ujenzi wa barabara hiyo kwa Serikali na Kampuni yao wakati swa ufunguzi wa barabara hiyo mpya na ya kisasa Wete Gando.
Rais Waziri wa Miundombinu na Mawasiliano Zanzibar Mr. Issa Haji Gavu akizungumza na kumkaribisha Rais wa Zanzibar kuzungumza na Wananchi wa Gando wakati wa hafla ya ufunguzi wa barabara hiyo. uliofanywa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein,

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein, akiwahutubia Wananchi wa Gando wakati wa hafla ya uzinduzi wa barabara mbili za Wete Gando Wete Konde, zilizojengwa na Kampuni ya Mecco Tanzania.
Wananchi wa Jimbo la Gando wakifuatilia hafla hiyo ya uzinduzi wa barabara yao. uliofanywa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein.
Wananchi wakimsikiliza Rais wa Zanzibar wakati akiwahutubia baada ya uzinduzi wa barabara hizo huko Wete Pemba. 
 Baadhi ya Wananchi wa Wilaya ya Wete Pemba wakifuatilia hutuba ya Rais wa Zanzibar wakati wa hafla ya Uzinduzi wa Barabara hizo.


Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein, akiitikia dua baada ya kumalizika kwa hafla za uzinduzi wa barabara.
Viongozi wa Serikali wakiitikia dua wakati wa kumalizika hafla ya uzinduzi wa barabara uliofanywa na Rais wa Zanzibar.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.