TAARIFA YA MGAO WA UMEME
Shirika la umeme
Zanzibar limesema kuwa kuanzia kesho alhamis kutakua na mgao wa umeme wakati wa
mchana utakaodumu kwa muda wa siku kumi na tano kisiwani Unguja.
Kwa mujibu wa
taarifa iliyotolewa na Shirika hilo imesema kuwa mgao huo utakua ni wa masaa
mawili na nusu kwa laini zitakazohusika na utakuwa kwa siku za Jumanne na Alhamis.
Taarifa hiyo
imefafanua sababu ya mgao huo ni kutokana na majaribio ya kuunganishwa gridi ya
taifa na mitambo ya gesi ya Kinyerezi majaribio yanayofanyika huko Tanzania
bara.
Taarifa hiyo
imezidi kufafanua kuwa kutokana na majaribio hayo kutapelekea kuzimwa mitambo
inayotumika sasa jambao ambalo litapelekea kupatikana kwa kiwango kidogo cha
umeme.
Majaribio hayo
yanatarajiwa kufanyika kuanzia saa 2 asubuhi hadi saa 12 jioni kwa siku za Jumanne na Alhamis.
No comments:
Post a Comment