Habari za Punde

Uwekaji wazi wa daftari la awali la wapiga kura katika mikoa ya Unguja na Pemba




JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

TUME YA TAIFA YA UCHAGUZI

TAARIFA KWA UMMA

UWEKAJI WAZI WA DAFTARI LA AWALI LA WAPIGA KURA KATIKA MIKOA YOTE YA UNGUJA NA PEMBA.

Tume ya Taifa ya Uchaguzi inatarajia kuweka Wazi Daftari la Awali la Wapiga Kura katika Mikoa yote ya Unguja na Pemba kuanzia tarehe 03/09/2015 hadi tarehe 07/09/2015 ili Umma uweze kupata nafasi ya kulikagua Daftari la Awali na kutoa taarifa za kufanyiwa marekebisho pale inapostahili.

Tume ya Taifa ya Uchaguzi, inaomba wananchi wote wajitokeze kukagua Daftari hilo litakalowekwa wazi katika Ofisi za Shehia, na ili kurekebisha taarifa za Wapiga Kura BVR Kit zitawekwa katika ofisi za Wilaya. Wakati wa uhakiki Mpiga kura anaweza kuhakiki taarifa zake kutumia simu ya mkononi  kwa kuingiza *152*00# au tovuti ya Tume www.nec.go.tz kisha wafuate maelekezo, ili kama kuna mapungufu yaweze kufanyiwa kazi kabla ya kuchapisha Daftari la mwisho litakalotumika siku ya Uchaguzi.


Imetolewa na Mkurugenzi wa Uchaguzi

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.