Kwa
miaka mingi upatikanaji wa wataalamu wa Afya na matibabu ya uhakika unakabiliwa
na changamoto kuu mbili inayowakumba wagonjwa wengi Tanzania.Watanzaniawamekuwa
wakisafiri nje ya nchi kupata matibabu ya Figo na magonjwa yanayohusiana na
kibofu.
Hivyo wataalamu wawili waliobobea katika magojwa ya Figo na Kibofu kutoka Hospitali za Apollo walitembelea nchini Tanzania wakishirikiana na madaktari kutoka Hospital ya Hindu Mandal ili kuwafanyia uchunguzi, kutoa tiba na kutoa ushauri kwa wagonjwa mbalimbali Tanzania.
Dkt V. Rajagopal ambaye ni mtaalamu wa magonjwa ya njia ya mkojo na mfumo wa uzazi wa kiume na amekuwa mshauri mwandamizi wa magonjwa ya kibofu katika Hospitali za Apollo huko Hyderabad India tangu mwaka 1994. Dkt. Sanjay Maaitra ambaye ni mtaalamu wa magonjwa ya Figo kwa kutoa huduma za matibabu ya figo na magonjwa yanayoambatana na Figo ikiwa lengo kuu la ujio wao ni kuhakikisha wagonjwa wanapata uchunguzi sahihi bila kuingia gharama kubwa za kwenda nje ya nchi.

Wagonjwa
wanaosubuliwa na magonjwa yanayohusiana na figo pamoja na mkojo walihudhuria na
kushiriki katika tukio hili. Madaktari
hao waliwafanyia wagonjwa uchunguzi kwa kupitia taarifa zao nyuma na kuzipitia
upya, kutoa historia ya matibabu na kutoa ushauri wa matibabu na tiba kwa
wagonjwa wapya waliojitokeza.
Kama
ilivyoelezwa hapo juu lengo la ujio wa madaktari hawa ni kupata taarifa za
wagonjwa wote ambao walipata huduma za matibabu kutoka kwao iwe ndani ya nchi
au katika Hospital za Apollo huko Hyderabad. Lengo la Dkt. Rajagopal na Sanjay Maitra
ilikuwa ni kuangalia jinsi gani wagonjwa wao wamepata nafuu na kama wanahitaji
vipimo zaidi na marekebisho ya tiba.
Kwa mfano mgonjwa ambaye amepandikishwa figo anahitaji muda mrefu wa ushauri na uchunguzi wa mara kwa mara. Ujio wa madokta hawa hapa nchini umekuwa jambo jema kwa kuwa umewarahisishia wagonjwa kupata matibabu kwa urahisi na uchunguzi wa muda mfupi. Endapo kama afya za wagonjwa zilitambulika kuzorota hivyo madaktari walipendekeza wapate vipimo zaidi katika Hospitali za Apollo, Hyderabad au Hospitali zozote zile.

Taasisi ya Upandikizaji ya Apollo (ATI), ni sehemu ya Hospitali za Apollo ambayo niTaasisi kubwa na imara katika mpango wa upandikizaji figo duniani. Wanatoa huduma za uchunguzi wa figo, Ini, Upandikizaji figo, upandikizaji wa ‘Corneal’ ‘GI’, matibabu ya tumbo na huduma nyinginekwa watoto. Taasisi hii inatoa ushari mbalimbali, vipimo na tiba.
Wakati wa ujio wa madaktari, tulipata fursa ya maohijiano na Dkt. V. Rajagopal pamoja na Dkt. Sanjay Maitra, tuliwauliza kama wameona mabadiliko yoyoteya afya Tanzania tangu walipokuja safari yao ya mwisho.
Pia madaktari hawa walitaja idadi ya wagonjwa ambao waliofika katika kliniki na kuona idadi kubwa kuongezeka kutokana na watu kutambua upatikanaji wa huduma hizo na mafanikio ya watu waliowahi kutibiwa na kushauriwa na madaktari hao wa kimataifa wenye ujuzi mkubwa.
Hata hivyo Watanzania bado wanakosa njia za kupambana na magonjwa haya tangu mwanzo. Madokta walikuwa na maoni kwamba, mwamko utaongezeka kama watu wanatapata elimu ya kutosha kutoka kwa madaktari juu ya uzuiaji wa magonjwa haya kwa kutambua dalili za mwanzo.
Daktari. V. Rajagopal na SanjayMaitra walisisitiza umuhimu kuzuia magonjwa haya na pia kufanya vipimo mara kwa mara. Waliendelea kusema kwamba magonjwa haya huwapata hasa watu wenye umri mkubwa lakini pia huweza kuzuilika.
Watanzania wanatakiwa kuwa makini kutokana magonjwa mengi yanayotokana na figo hasa kwa watu wazima ni kutokana na Shinikizo la Damu, Kisukari, wingi wa Lehemu, kutofanya mazoezi, Ulaji mbaya pia utumiaji usio sahihi wa dawa hasa za kutuliza maumivu. Hivyo husababisha ulemavu wa figo.
Pia Dkt. Sanjay Maitra alitoa ushauri ni vyema kuzingatia vipimo mara kwa mara kwani inasaidia watu kujua afya zao.Alitoa mfano wa mtu mmoja, ambaye ni dereva mwenye ujuzi wa miaka hamsini na kipindi chote alikuwa anaumwa miguu na mwishowe aligundulika kuwa na kisukari kwa miaka kumi na tano.
Pia mgonjwa huyo hakujua kuhusu shinikizo la damu wala hakuwa na walipompima walimgundua hana uwezo wa kuona vizuri. Dkt. Sanjay Maitra aligundua kuwa ana ugonjwa wa kisukari. Pia kwa bahati mbaya pia watanzania wengi wanashabihiana na mfano huo kwa kuwa hawajui dalili mwanzo za magonjwa haya.
Aliongeza kwa kusema kuwa ni muhimu kwa wao kutembelea kwani wameleta mwamko mkubwa.Pia Madokta hawa wametoa wito kwa Watanzania kupata taarifa zaidi juu ya kupambana na magonjwa haya ili kuishi kwa afya njema na maisha marefu.
Tukio hili la madaktari kutembelea taasisi za afya hapa nchini lengo ni kuleta ushirikiano katika huduma za afya na mafunzo kwa madaktari wa hapa nchini.
Dkt. Sanjay Maitraamesema ni jambo gumu na linahitaji hela
nyingi kwa wagonjwa kusafiri nje ya
nchi, hivyo yeye ameona ni vyema kuweka muda ili kuja kutoa huduma kwa ukaribu zaidi. Anatumaini kwamba wagonjwa watatibiwa kwa
urahisi hata wakiwa nje ya nchi.
Lengo
la ujio wao si kwamba kuwachukua wagonjwa na kuwatibia katika Hospitali za
Apollo bali ni kuwapa ushauri sahihi na kuwasaidia kufanya maamuzi sahihi ya
matibabu. Mbali na suala la wagonjwa lakini tumeona pia wachache kati yao wataweza
kwenda Apollo kama watahitaji matibabu.
Alipoulizwa kuhusu watanzania watakachopata wakienda Hospitali za Apollo, Dkt. V Rajagopal alisema kwamba mpango wa Kimataifa wa Apollo ni kusaidia wagonjwa na washirika wao ili kurahisisha huduma za afya.
Pia wanatoa ratiba ya uteuzi, usafirishaji, na huduma za ukalimani kwani Hospitali za Apollo pia zinatoa huduma ya ukalimani kwa lugha ya Kiswahili ili kuwahudumia wagonjwa wanaotoka Kenya, Uganda na Tanzania kwa urahisi. Hospitali za Apollo zinajulikana kwa kwenda mbali zaidi kuwafanya wagonjwa kuhisi unafuu.
Mwaka
2014, Mji wa Apollo (Apollo Health City) Hderabad, ulipata tuzo ya heshima ya KIMATAIFA
YA MATIBABU NA UTALII kutoka Jarida la
Kimataifa la Matibabu na Usafiri
kutokana na utoaji wa huduma bora kwa wateja.
Hospitali za Apollo zinamfanya mgonjwa ajisikie kama yupo nyumbani kwani huwaandalia wagonjwavyakula vikuu kama ugali, ndizi mtori, ingawa wagonjwa wengi wa kiafrika wanapenda kujaribu vyakula vya kihindi. Pia mapishi yanaenda mbali zaidi kwa kuandaa chakula cha watoto na watu wazima. Chakula ni muhimu sana kwa wagonjwa ili kuwa na afya. Hospitali za Apollo zinaamini kwamba “kama tunafahamu chakula basi pia tunafahamu tamaduni husika”.
Kuhusu
Apollo:
Mnamo mwaka 1993, Dkt. Prathap C. Reddy,
mbunifu wa afya nchini India, alianzisha hospitali ya kwanza ya ushirika nchini
India, Hospitali za Apollo Chenai. Kwa miaka mingi, Hospitali za Apollo
zimeweza kukua kufikia moja ya shirirka kubwa la afya barani Asia likiwa na
uwezo wa zaidi ya vitanda 8,500 ndani ya Hospitali 50, zaidi ya maduka 1350 ya
dawa na zaidi ya kliniki za uchunguzi 100.
Pia hospitali za Apollohutoa huduma za matibabu kwa utaratibu wa kibiashara, huduma za bima za afya na kitengo cha tafiti za kitabibu kwa lengo la kufanya tafiti za magonjwa ya milipuko, seli shina za mwili na maumbile. Kuendeleza vipaji ili kumudu hitaji linaloongezekaa katika utoaji huduma za hali ya juu,
Hospitali za Apollo zina jumlaa ya vyuo 11 vya madaktari pamoja na wauguzi. Mafanikio haya yamezifaidisha Hospital za Apollo kupata tuzo mbali mbali, ikiwa ni pamoja na tuzo ya kituo bora iliyotolewa na serikali ya India pamoja na kutambulika na tume ya pamoja ya kimataifa ( Hospitali saba za Apollo zinatambuliwa na kutunikiwa na tume ya pamoja ya kimataifa). Katika hesima nadra, serikali ya india ilitoa mhuli wa kumbukumbu wa kuutambua mchango wa Hospitali za Apollo Dkt.
Prathap C Reddy, alitunukiwa tuzo ya heshima ya Padma Vbhushan’ mnamo mwaka 2010. Ushirika wa Hospitali za Apollo kwa zaidi ya miaka 50, umeendelea kuboresha uongozi katika uvumbuzi wa kitabibu, huduma za kimataifa na maendeleo ya kiteknolojia. Hospitali zetu zimekuwa katika nafasi ya juu kimatifa katika huduma za kitabibu pamoja na utafiti.
Gadiel E.W. U (Gadiola Emanuel)
IT/ PR /Photojournalist /Event Planner / Photographer (Northern Shots ) and Blogger -Based in Arusha, Tanzania.
Mob :+255 715 /755 643 633
E-mail: gadiola25@gmail.com
WEB: www.wazalendo25.blogspot.com
: www.arushapublicity.com
:www.northernshotstz.com

No comments:
Post a Comment