Habari za Punde

Mgombea Urais wa Chama cha TLP Achukua Fomu ya Urais wa Zanzibar.


Mkurugenzi wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar ZEC Ndg Salum Kassim Ali akizungumza wakati wa kukabidhi fomu za Urais wa Zanzibar kwa Mgombea wa Chama cha TLP Mhe. Mhe Khafidh Hassan Suleiman, katika Afisi za Tume ya Uchaguzi bwawani hoteli. 
Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar ZEC Mhe Jecha.S.Jecha akisoma fomu ya kugombea Urais wa Zanzibar kabla ya kumkabidhi mgombea wa Chama cha TLP, hafla hiyo imefanyika Afisi za Tume ya Uchaguzi zilioko katika hoteli ya bwawani Zanzibar.  
Mgombea Urais kupitia Chama cha TLP Mhe Khafidh Hassan Suleiman, akiwa makini kusikiliza maelezo ya fomu ya kugombea Urais wa Zanzibar yakisomwa na Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Mhe Jecha.S.Jecha, akiwa na viongozi wa Chama hicho waliomshindikiza Afisi za Tume Bwawani Zanzibar.
Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar Mhe Jecha.S.Jecha akionesha mkoba wa Fomu za kuwania Urais wa Zanzibar kwa Wanachama wa Chama cha TLP waliofika katika Afisi za Tume ya Uchaguzi Zanzibar zilioko hoteli ya Bwawani Zanzibar 
Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar ZEC Mhe Jecha.S.Jecha akimkabidhi mkoba wa Fomu za kugombea Urais wa Zanzibar Mgombea Urais wa Chama cha TLP Mhe.Khafidh Hassan Suleiman.
Mgombea Urais wa Chama cha TLP Mhe Khafidh Hassan Suleiman, akionesha mkoba wake wa Fomu za kuwania Urais wa Zanzibar baada ya kukabidhiwa na Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar. 

Mgombea Urais wa Chama cha TLP Mhe Khafidh Hassan Suleiman, akizungumza na waandishi wa habari wa vyombo mbalimbali waliofika wakati wa hafla hiyo ya kuchukua fomu ya Urais na kutangaza Sera zake kwa waandishi wa habari Zanzibar.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.