Winchi laanguka katika msikiti wa Masjid al Haraam mjini Makkah hivi leo. Inasemekana zaidi ya watu sitini wamefariki na wengine wengi wamejeruhiwa.
Winchi hili limeanguka kutokana na upepo mkali uliokuwa ukivuma katika Msikiti wa Makkah pamoja na mvua iliyokuwa ikinyesha.
Mji wa Makkah tayari umeanza kupokea Mahujaaj kwa ajili ya kuitekeleza Ibada ya Hijja ambayo ni nguzo ya tano katika nguzo za kiislamu.
No comments:
Post a Comment